Naibu Waziri
wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mwalimu wa shule ya
Sekondari ya vipaji Maalumu ya Ilboru Mkoani Arusha mara baada ya kukutwa akiwa
amelewa wakati wa kazi shuleni hapo
Hatua hiyo
imekuja mara baada ya waziri huo kufanya ziara ya kawaida shuleni hapo kutafuta
ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi kupelekea kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa
na kugoma kuingia darasani hivi karibuni
Majaliwa
alilazimika kufanya hivyo wakati akiongea na walimu wa shule hiyo juu ya nini chanzo
cha mgogoro huo,ambapo mwalimu huyo,Potin Jovita Sumawe, alinyanyuka na
kuanza kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa mbele ya Waziri huyo
“Nimemuagiza
afisa utumishi kumpeleka hospitalini kwaajili ya kupimwa kama
anamechanganyikiwa na ripoti iliyoletwa kwangu nikuwa alikuwa amelewa hivyo
tunamsimamisha kazi na kuanza kupitia faili lake tuone kama anaweza kuonyeka
ama laa!”alisema Majaliwa
Aidha
aliongeza kuwa watumishi wote hawatakiwi kwenda kazini wakiwa wamekunywa au
wametumia kilevyi cha aina yeyote huku akisisitiza kuwa mahali pa kazi sio
mahali pa kunywa pombe kwa kufanya hivyo nikuvunja sheria ya utumishi wa umma
“Kama mtumishi
wa umma anavunja sheria kwa kunywa pombe kazini atachukuliwa sheria kwa kuwa
hata Yule mtoto aliyekabidhiwa kumfundisha anamfundisha kwa misingi ipi?wafanye
kazi kwa maadili mema”alisema Majaliwa
Aliongeza
kuwa hii sio hapa tu bali sehemu yeyote mfanyakazi wa serekalini au
sekta binafsi haruhusiwi kufanya kazi akiwa amelewa hivyo mtu yeyote
akikutwa hivyo anastaili kufukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment