Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Kaike Silaji.
Na Amina Athumani
OGANAIZESHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), imempa siku saba promota wa ngumi za kulipwa, Kaike Siraju au kumfikisha mahakamani endapo atashindwa kuwalipa mabondia chipukizi, Issa Omar na Mwaite Juma aliowapandisha ulingoni Julai 15, mwaka huu kwa makubaliano ya kuwalipa na baadaye 'kuingia mitini'.
Juni 25, mwaka huu Kaike aliwasainisha mkataba mbele ya Katibu Mkuu wa Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe kuwa Omar kucheza na Ramadhan Kumbele kwa malipo ya sh. 80,000.
Pia Kaike alifanya hivyo kwa bondia, Juma aliyecheza na Anthony Mathias, ambapo vijana hao walicheza na hawakulipwa na promota huyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamwe alieleza kuwa baada ya pambano Kaike alitoroka na mabondia walipojaribu kumdai haki yao kwa siku zilizofuatia walipigwa kalenda.
"Anawapiga kalenda mabondia na kuwatembeza tembeza kwa usumbufu kwakuwaambia wamfate mara yupo Mango Garden asubuhi na kuwagandisha mpaka jioni na kuwaambia njooni kesho Magomeni saa tano vijana walifika saa tatu na kuganda mpaka saa tisa walipompigia simu aliwaambia waachane naye wakati mwanzo alikuwa anawaambia wamsubiri sasa anawaambia waachane naye na kuwatisha" alisema Kamwe.
Alisema vijana hao waliripoti TPBO na kueleza madai yao, na kwamba TPBO walimpigia simu Kaike naye akakubali kuwalipa kupitia kwao na kusisitiza kuwa vijana hao wasimfuate.
Alisema kutokana na hatua hiyo TPBC inamtaka Kaike kuwalipa mabondia hao haraka iwezekanavyo kwa kuwa walikubaliana kwa mujibu wa mkataba alioingia nao.
Alisema mbali ya kutowalipa mabondia hao, bondia mmoja kati ya hao aliumia jicho katika mchezo huo hali iliyofanya wazazi wa kijana huyo kulalamika kwa uongozi kuwachezesha mabondia bila ya kuwalipa na kutowajali wanapopata majeraha.
Kamwe alisema mambo yanayofanywa na promota huyo si ya kiungwana na ni kuwavunja moyo mabondia chipukizi, ikiwa ni kudumaza ngumi na kufanya mchezo wa ngumi uonekane ni mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivyo.

1 comment:
Mteja anaposema huduma zako ni za hali ya chini (negative views) hana maana ya kukudhalilisha ila anakuomba ufanye improvements where necessary. Hata ukiona hotel za nyota tano, ni kutokana na positive views kutoka kwa wateja. Hiyo hotel iliruhusu Yanga kulala wachezaji wawili kitanda kimoja. Inawezekana sheria ya Tanzania inaruhusu, lakini it sounds weird internationally. You cannot assign two unrelated adults a single room halafu unapokosolewa unakuja juu. Tukitaka maendeleo lazima tujifunze good customer service. Tumuone mteja kama rafiki na siyo adui maana anapoondoka hapo hotelini atakwenda kuelea ubaya au uzuri wa huduma zetu.
Post a Comment