Baada
ya msanii anae-make headlines za kutosha Diamond Platnumz weekend
iliyopita kukanusha habari zilizochapishwa na gazeti la Risasi kuwa
ana mahusiano mapya ya kimapenzi na binti kutoka Kenya, sasa
amefunguka tena kuhusiana na yeye na Wema Sepetu kupitia website yake.
"Najua
watu wengi sana mnapenda Couple hii na furaha yenu ni kutuona wawili
sisi tukiwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.... na mmekua mkifurahi sana
na story za hapa na pale mkiskia kua wawili sisi tumekua pamoja na hata
pindi mkituona tuko pamoja pia Mmekua mkishangilia na kufurahi...
bt
ukweli ni kwamba Mimi na Wema hivi sasa si Wapenzi tumekua ni kama
Dada na Kaka ama marafki tu wa kawaida ambao tunashirikiana katika kazi
mbalimbali za sanaa na za n'nje ya sanaa, katika harakati za kujenga
Taifa Letu... Pia ni vizuri ningependa mfahamu kwamba Wema ana Mpenzi
wake ambae namfaham na tunaheshimiana kama mtu na Shemeji
yake........So das' de Truth abt me and Her!... and Get ready! kwa kazi
tofautitofauti ambazo soon zitadondoka....".
Habari ndio hii!!!
1 comment:
haya tumekusikia mheshimiwa kadogo kwamba wewe na wema sasa hivi ni kama kaka na dada na wema anaye wake mnafanya kazi pamoja tu alright bora ya hayoo kwa sababu wema ataachiwa radhi za wazee wake akikufuata fuata sana
mdau NY
Post a Comment