ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 19, 2012

SIMBA, YANGA KUKABIDHIWA MABASI YAO IJUMAA KWA BONGE LA SHEREHE... WATAONDOKA NAYO KWA MISAFARA KUPITA KATIKA MATAWI YAO KWA MUZIKI

Hatimaye, yale mabasi waliyoahidiwa Simba na Yanga kutoka kwa mdhamini wao yapo karibu kukabidhiwa, kwa sasa yakiwa kwenye hatua za kupambwa rangi za klabu hizo, Hili ni basi la Yanga ambalo bado kubandikwa nembo tu ya klabu na jina. Basi la Simba pia litakuwa hivi, tofauti rangi. Hongera TBL, Simba na Yanga wanatakiwa kuyatunza vema magari haya, kuhakikisha wanayafanyia service mara kwa mara, yanakuwa katika hali nzuri kila wakati. 
Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

No comments: