ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 19, 2012

SIMBA RAHA TUPU KILELENI, YAWATANDIKA MAAFANDE WA JKT RUVU


SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanania Bara, baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya kucheza pungufu baada ya Emanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mabao ya Simba yalitiwa kimiani na viungo Amri Kiemba na Haruna Moshi ‘Boban’ na kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza ligi kwa kufikisha pointi sita, baada ya awali kuifunga African Lyon 3-0.  
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo, Mrisho Ngassa na Emanuel Okwi. Matokeo mengine yanakuja.

No comments: