Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa shukurani kwa Wadhamini wakuu waliofanikisha Serengeti Fiesta 2012 kufanyika na kumalizika kwa amani kwa mikoa takribani 12 nchini Tanzania ilhali tamasha hilo likiacha alama ya maendeleo na chembe za changamoto ya ukuzaji uchumi kwa wananchi wa mikoa iliyo kuwa kwenye ratiba.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki Bora kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL),Steve Gannon ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kupitia bia yake maridhawa kabisa ya Serengeti Premium Lager pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo ya SBL,Ephraim Mafuru.Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye kiota cha maraha cha Escape Two,Mbezi beach jijini Dar.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki bora kwa wadhamini wa mafuta vyombo vya barabarani GAPCO walioshiriki vyema Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwa Mkuu wa Masoko wa GAPCO, Ben Temu.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya SBL, Ephraim Mafuru akitoa shukurani za dhati kwa wadau mbalimbali waliofanikisha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwa namna moja ama nyingine.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Sir Juma Nature akimwimbia mmoja wa watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo. Katika hafla hiyo iliyokuwa ya aina yake iliwajumuisha watu mbalimbali wakiwemo wasanii mbalimbali walioshiriki tamasha la serengeti fiesta 2012 na wadau wengine.
PICHA NA : gsengo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment