ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 20, 2012

HALI TETE MJI WA GOMA:

Watu wakikimbia mapigano ya waasi katika mji  wa Goma nchini Congo mji huo una utajiri mkubwa wa madini 

Wapiganaji hao walifanikiwa kuudhibiti baada ya mapambano makali yanayoendelea kati ya waasi na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

WAPIGANAJI wa Kundi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo leo wameudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma.

Wapiganaji hao walifanikiwa kuudhibiti baada ya mapambano makali yanayoendelea kati ya waasi na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Hali hiyo imetokea wakati ambapo Rwanda inavituhumu vikosi vya jeshi la Kongo vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa kulishambulia eneo lake wakati wa mapambano na waasi karibu na eneo la mpakani hapo jana.
Chanzo:Mwananchi

No comments: