Hawa jamaa wa UN wasitake kutuchezea akili. Adhabu ya kifo ni mbaya, sawa; lakini inastahili. Nimepata kumhoji Jaji Samatta juu ya adhabu hiyo. Yeye anaiunga mkono. Hoja yake ni kwamba kuna kesi ukiisikiliza, ukajua namna mhusika alivyoshiriki kumuua binadamu mwenzake, kama kweli ni Jaji mtenda haki, atamhukumu adhabu ya kifo. Juzi hapa wanajeshi wamehukumiwa kifo kwa kumuua Swetu. Hawa watu ukiwakuta mitaani wanavyoadhibu binadamu wengine hadi kuwaua, hakika huwezi kuwaonea huruma nao wanapohukumiwa.
Fikiria, majambazi wanaingia nyumbani kwako na kuiua familia yako, kisha wanaambulia kuchukua sh laki moja, au kuku, au mbuzi. Katika mazingira kama hayo, wahusika wakipatikana hakuna adhabu sahihi kwao zaidi ya kunyongwa, tena si kunyongwa tu, bali kunyongwa hadi kufa.
Kama kweli UN wanaona adhabu hii haifai, basi waanze na wafadhili wao wakuu, "mabwana" wa demokrasia-Marekani ili nao waache kufanya hivyo. Saddam Husseina alinyongwa, Gaddafi kauawa na wakala wao Wamarekani na Wafaransa; iweje kuwaua hawa iwe halali, lakini sisi kuwanyonga wanaowanyonga ndugu zetu iwe si haki?
Afrika Kusini walijipendekeza kufuta adhabu hiyo kwa busara zas Jaji Mwalusanya wa Tanzania. Sasa wanajuta! Wanataka adhabu ya kifo irejeshwe maana ushenzi umepindukia nchini humo.
iTuache kuimba wimbo wa UN pamoja na asasi za kiraia ambazo kazi yake ni kusaka fedha. Adhabu ya kifo inawafaa sana wale wanaoistahili. Haki ya kuishi isiwe kwa muuaji tu, bali tutazame na yule aliyeuawa anatendewa haki vipi!
Manyerere
Nawasilisha
1 comment:
Nayaheshimu maoni yako japokuwa yako more emotional than rational. Kwa maoni yangu, zipo sababu nyingi nzuri dhidi ya adhabu ya kifo, zikiwemo zifuatazo:-
(1) Hakuna judiciary system hapa duniani ambayo ni perfect. Wapo watu wengi ambao walinyongwa, lakini baadaye ikagundulika kwamba actually walinyongwa kwa makosa ambayo hawakuyafanya.
(2) Hakuna ubishi kwamba kuua ni kosa kubwa. Why should a state be drawn into committing the same sin? Huwezi ukasahihisha kosa moja kwa kufanya kosa jingine (tena la aina hiyo hiyo). Isitoshe, lengo la adhabu ni kumrekebisha mtenda kosa. Unaweza ukashawishika kuamini kuwa faida ya adhabu ya kifo ni kutoa fundisho kwa wengine, lakini imani hiyo pia siyo sahihi, kama ninavyobainisha katika sababu inayofuata.
(3) Zipo tafiti nyingi zilizofanywa na criminologists na watafiti wengine zinazoonyesha kwamba homicide rate kwenye nchi au state zenye adhabu ya kifo is not necessarily lower than that in countries or states with no capital punishment. Kwa mfano, homicide rate katika state ya Texas (ambako ni makao makuu ya capital punishment) ni kubwa kuliko homicide rate katika nchi ya Sweden (ambako hakuna capital punishment).
Etc.
Post a Comment