ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 2, 2012

JB MPIANA JUKWAA MOJA NA H.BABA, MB DOG NA NEY WA MITEGO NOVEMBA 30

Mkurugenzi wa Kampuni ya QS, Joseph Muhonda, akiongea kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Novemba 30.
Wanamuziki wa kizazi kipya cha Bongo Fleva, Hamis Ramadhani ‘H.Baba na Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ wakisikiliza jambo fulani kwa makini
Mratibu wa tamasha hilo, King Dodoo (wa kwanza kushoto) na Muhonda akiwasikiliza waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo.

NA IMELDA MTEMA, GPL
KAMPUNI ya QS Muhonda J Entertainment iliyozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam hivi kribuni, itamleta mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, JB Mpiana, ambaye atafanya onyesho la aina yake Novemba 30 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Muhonda, alisema wanamuziki watatu wakali wa Bongo Flava ambao ni Hamisi Ramadhani ‘H. Baba’, Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ na Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ ambao wako chini ya kampuni yake, wataungana na mwanamuziki huyo katika onyesho hilo.
Pia alisema Bendi ya Mashujaa itashiriki katika burudani hiyo ya kukata na shoka.                               

No comments: