ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 20, 2012

KESI YA LULU DESEMBA 3


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha leo kesi inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika. 
Hata hivyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala aliomba mahakama kuhimiza upande wa mashtaka kuongeza kasi ya upelelezi kwa kuwa mshtakiwa anateseka mahabusu.
Hakimu Mkazi Augustina Mmbando alisema upande wa Jamhuri ukamilishe upelelezi na kesi hiyo itatajwa Desemba 3 mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba.
Aidha, kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji lakini mara upelelezi wake utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

No comments: