Serikali imezidi kuandamwa na sakata la utoroshwaji nje wa mabilioni ya fedha, baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kubanwa bungeni akitakiwa kueleza hatua zilizochukuliwa na serikal;I kurejesha nchini fedha hizo za walipa kodi.
Baada ya jana kubanwa na kutakiwa kueleza uchunguzi wa fedha hizo ulikofikia, Pinda aliliambia Bunge kuwa serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa madai ya kuwepo kwa mabilioni ya fedha za kigeni zilizotoroshwa nchini na kufichwa kwenye mabenki ya ughaibuni na kwamba uchunguzi huo ukikamilika, taarifa za majina ya wahusika, hatua zitakazochukuliwa dhidi yao na mkakati wa kurejesha fedha hizo itatolewa kwa wananchi.
Alitoa jibu hilo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua hatua na mkakati uliochukuliwa na serikali kuhusu suala ikiwamo kuwataja wahusika.
Mbowe alisema fedha hizo zimehifadhiwa kwenye akaunti za viongozi waandamizi, viongozi wastaafu na wafanyabishara kinyume cha sheria na kanuni za nchi, na alisema tangu wakati wa Mkutano wa Bajeti kwa mwaka 2012/13 zilipotolewa tuhuma hizo, serikali bado imekuwa kimya kuzungumzia hatua ilizofikia katika kulishughulikia suala hilo.
“Ni kweli niliahidi kutoa taarifa ya jambo hilo kwa sababu ya ukubwa wake, nilisema tutahitaji kufanya uchunguzi wa kina na hilo jambo tunalifanya na tutatoa taarifa,” alisema Pinda.
Katika swali la nyongeza, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema), alitaka kujua kwa nini serikali haijaamua kuomba kibali kwa Benki ya Dunia kupitia kitengo chake cha kurejesha mali (Asset Recovery Unit) ili kisaidie kurejesha fedha hizo ambazo zimefichwa sio Uswisi pekee, bali katika nchi nyingi kama vile Dubai, Jersey, Grenada, Luxemburg, Mauritius na nchi zingine kwa vile nchi hizo hazitozi kodi.
Mbowe alitoa hoja hiyo akionyesha wasiwasi kuhusu uchunguzi unaofanywa kwa kuhusisha vyombo vya hapa nchi ambavyo alidai vinaweza kuwalinda wahusika.
Pinda alisema: “Mheshimiwa Mbowe anaweza kulirudia suala hili mara mbili tatu, na mimi nitajibu hivi hivi kwamba uchunguzi bado unaendelea na utakapokamilika tutatoa taarifa.”
“Haiwezekani suala zito kama hili lenye tuhuma nyingi likaweza kupatiwa majibu ndani ya wiki moja, nasisitiza kwamba bado tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika tutawaeleza hatua stahiki zilizochukuliwa,” aliongeza.
Jumanne wiki hii, wakati wabunge wakichangia Azimio la Kuridhia Marekebisho ya Pili ya Mkataba wa Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki, (ACP), Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alitaka nchi za Umoja wa Ulaya (EU), zisaidie kurejeshwa kwa mabilioni ya fedha zilizoibwa, kutoroshwa na kufichwa kwenye mabenki ya Uswisi.
“EU ihakikishe mabilioni yaliyopelekwa kwenye mabenki ya Uswisi yanarejeshwa,” alisema.
Alisema katika kifungu cha 29 cha ACP, kinazungumzia ushirikiano wa kikanda katika kupiga vita rushwa na mambo mengine, sasa serikali imejipanga vipi kuhakikisha kwamba fedha zilizofichwa huko Uswisi zinarejeshwa nchini.
Hoja ya kufichwa kwa mabilioni ya fedha katika benki za Uswisi kulikofanywa na baadhi ya vigogo serikalini, ilifichuliwa kwa mara ya kwanza na Chadema na katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2012/13.
Waziri Kivuli wa Fedha wa Kambi ya Upinzani, Zitto Kabwe aliitaka serikali kuwataja kwa majina vigogo waliohusika na utoroshaji wa fedha hizo Sh. bilioni 300 la sivyo, kambi ya upinzani bungeni itawataja.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema wakati umefika kwa serikali kuliambia Taifa hatua itakazochukua kurejesha fedha hizo na nyingine zozote zilizopo ambazo imezifichwa ughaibuni.
Zitto mara kwa mara amekuwa akitishia kuwa ikiwa serikali itaendelea kuficha ukweli huo na kuchukua hatua, atawataja vigogo hao kwa majina.

CHANZO: NIPASHE
2 comments:
Safi sana viva chadema
Huo uchunguzi utaendelea hadi lini?si uongo tu wanalindana ili ukweli usijulikane!
Post a Comment