ALIYEKUWA mume wa msanii wa filamu, Nuru Nassoro ‘Nora’, Masoud Ali ‘Luqman’ amesema ni kweli ndoa yao imevunjika muda mrefu uliopita ila sababu ya kuachana kwao ni aibu endapo ataitaja. Akizungumza na Ijumaa baada ya habari ya Nora kupewa talaka kuripotiwa, Luqman alisema kumekuwa na maneno mengi yanayosemwa na watu kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa yao lakini yote si ya kweli ila siku akiamua kuitaja sababu, Nora hatatembea mtaani kwa aibu.
“Ni kweli ndoa imevunjika, tumekuwa tukiachana mara kwa mara na kurudiana lakini safari hii imekuwa ni moja kwa moja kwani mimi nina mtu wangu mwingine na yeye nasikia ana mtu wake.
“Kinachonikera ni sababu zinazotajwatajwa kuwa ndizo zilizosababisha kuachana kwetu kwani si za kweli, mimi ndiyo nina sababu na sababu zenyewe nikizianika itakuwa ni aibu kwa Nora, Nora anyamaze na aendelee na maisha yake na kama ana ujasiri aseme yeye kwa nini tumeachana…” alisema Luqman.
Nora na Luqman walifunga ndoa mwaka juzi ambayo
imedumu miezi 24 tu.
No comments:
Post a Comment