Kama kawaida ya JB. Mpiana humtegemea mungu kwa kila jambo, hapo akimuomba mungu.
Mwanamuziki nguli wa mambo ndombolo ya solo, JB MPIANA (kushoto) sambamba na Kosovo wakitoka nje ya uwanja wa Mwalimu Nyerere jijin Dar es salaam.
Usafiri wa nguvu uliokuja kumchukua Mwanamuziki JB Mpiana
JB Mpiana Akiongea machache na Mwenyeji wake Joseph Mhonda
Sambamba na wacheza shoo wake mahiri wadada wamekamilika, patakuwa hapashi pale tarehe Nov.30.
Mwanamuziki JB Mpiana akiongea na mwandishi wa habari
Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo JB Mpiana, aliwasili jana 26Nov. mida ya saa mbili za usiku ktk uwanja Mwalimu Nyerere jijini Dar, tayari kwa maonyesho ya nguvu. Mwanamuziki huyo anatarajiwa kufanya onyesho la pamoja na bendi ya Mashujaa katika Viwanja vya Leaders Novemba 30. Alipokelewa Mkurugenzi wa Q. S. Joseph Mhonda
Picha zote na Issa Mnally
No comments:
Post a Comment