ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 1, 2012

Ommy Dimpoz Atangaza Kumsamehe Lord Eyez Kwa Kumwibia



Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amesema kuwa licha ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kurudisha gari yake kwenye hali ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez anayeshikiliwa korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka kwenye gari yake.

Akizungumza na mtandao huu mapema leo Ommy Dimpoz amefunguka kuwa ingawa kwa sasa haruhusiwi kusema lolote kuhusu jambo hilo lakini anayo haki ya kusema kuwa binafsi amesamehe na anamuachia Mungu.

“Nafahamu kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote kwa kuwa suala liko Polisi,ninachoweza kukwambia ni kuwa binafsi nimemsamehe Lord na wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga kukutana naye na kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumiatena licha ya kuwa nimetumiagharama kubwa” alisema Dimpoz.

Katika hatua nyingine nyota huyo wa songi la ‘Badae’ ameanika kuwa wimbo huo umemuingizia kiasi kikubwa cha pesa tofauti na yalivyokuwa matarajio yake huku pia akijikusanyia wingi wa marafiki ndani na nje ya nchi kupitia wimbo huo.

No comments: