Original: English
RIPOTI YA NCHI MASIKINI SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA TARAKIMU
Geneva, 26 Novemba 2012 – Ripoti ya
Nchi Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121, yenye kichwa
kidogo cha habari Kutumia Fedha
Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa
Uzalishaji, imetolewa leo.
Mwelekeo wa uhamiaji
Ø Idadi
ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs) iliongezeka
kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010. Hii ni sawa na 3.3%
ya wakazi wote wa nchi hizo.
Ø Nchi
Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya
wahamiaji duniani kote---idadi ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi
ya wakazi wote duniani (12.1%).
Ø Wahamiaji
wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea (Kusini) na
mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha
Ø Kiwango
cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao
kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni 3.5
kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea
kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi duniani.
Ø Mwaka 2011 kiasi cha fedha zilizotumwa
kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka
Canada dola milioni 3.2 na kutoka Kenya dola milioni 2.5.
Ø Mwaka
2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani ya
uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15), na kiwango
hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi
Kutoka Nje, yaani ODA (dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha
fedha kutoka nje ya nchi.
Ø Kiwango
cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja mmoja
kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30 kati ya mwaka
2000 na 2010.
Ø Fedha
zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs ikilinganishwa
na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha zinazotumwa na raia
kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya thamani ya bidhaa
zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu ikilinganishwa na nchi
nyingine zinazoendelea (ambazo siyo LDCs).
Ø Kuanzia
mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo kinalingana
na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za Lesotho, Samoa, Haiti na
Nepal.
Ø Tangu
mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za nje
kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata
kutokana na mauzo ya bidhaa nje.
Ø Kwa
LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi kile
cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi
za Bangladesh, Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen.
Kwenye nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha
zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros,
Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.
Ø Theluthi
mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka
kwenye nchi zinazoendelea.
Ø Duniani
kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha fedha kilichotumwa;
kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja (12%).
Ø Kama
nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za uhamishaji fedha
kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato yao yangekuwa
yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka
2010.
Ø Asilimia
66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na 2011 ni za
nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na Sudan.
Ø Matumizi
ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi 1,000) kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa
wakazi 1,000). Simu za mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na
kupokea fedha kutoka ng’ambo.
Kuhama kwa utaalam
Ø Mtu
mmoja kati ya kila watu watatu wenye ujuzi mkubwa (mwenye elimu ya chuo kikuu)
kutoka LDCs anaishi ng’ambo. Kwenye nchi zilizoendelea kiwango ni mtu mmoja
katika kila watu 25.
Ø LDCs
sita zina raia wao wataalaum wengi zaidi wanaoishi nje ya nchi kuliko wale
waliobakia nchini mwao: Haiti, Samoa, Gambia, Tuvalu na Sierra Leone.
Ø Theluthi
mbili ya wahamiaji wenye ujuzi mkubwa kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi
zilizoendelea; theluthi moja wanaishi katika nchi zinazoendelea.
Ø Kiwango
cha kuhama kwa watu wenye ujuzi kwenda ng’ambo ni kikubwa (20% ) kwa LDCs
nyingi (30 kati ya 48).
Ø Wahamiaji
kutoka LDCs wenye elimu ya chuo kikuu ambao wanaishi na kufanya kazi ng’ambo
inafikia milioni 2.
Ø Idadi ya Watanzania waliohamia
Uingereza kwa kumbukumbu za mwaka 2000 ni 10,535.
Ø Aina
ya wahamiaji inafuata ukubwa wa kipato wa nchi mwenyeji. Katika nchi
zilizoendelea, 35% ya wahamiaji ni wale wenye elimu ya chuo kikuu; kwenye LDCs
4% tu ya wahamiaji wana kiwango hicho cha elimu. Viwango hivi ni kwa wahamiaji
kutoka nchi zote, japo viwango ni hivi hivi kwa wahamiaji kutoka nchi za kundi
la LDCs.
Ø Theluthi
moja ya wahamiaji kutoka LDCs ambao wana elimu ya chuo kikuu wanaishi Marekani.
Uwezo wa kiuchumi (Uchumi mpana)
Ø Kiwango
cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka kwa LDCs tangu kipindi cha msukosuko wa kiuchumi
duniani (2009-2011) ni 4.7%, ambacho ni chini ya kiwango cha kipindi cha miaka
ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi (2003-2008), yaani 7.9%. Hii ina maana kwamba
kiwango cha ukuaji wa kipato kwa mwaka kwa kila mkazi kilishuka kutoka 5.4%
miaka ya ukuaji mzuri wa uchumi hadi kufikia 2.4%.
Ø Wastani
wa ukuaji halisi wa pato la nchi katika LDCs mwaka 2011, yaani 4.2%, ulikuwa
chini ya 4.9% ya mwaka 2009 wakati wa anguko la uchumi duniani.
Ø Kile
kinachojulikana kama Gross fixed capital
formation kwenye LDCs kilipanda kidogo kutoka 20.7% ya pato la jumla la
taifa mwaka katika miaka ya 2005-2007 kufikia 21.6% miaka ya 2008-2010. Hata
hivyo, bado kilibaki chini ya viwango vya nchi nyingine zinazoendelea, ambazo
zilifikia kiwango cha 30.1%.
Ø LDCs
zinaendelea kutegemea sana raslimali kutoka nje. Pengo la pato linalotokana na
uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje lilikuwa kubwa kwa 20% ya pato la jumla la
taifa katika nchi tano za kundi la LDCs mwaka 2011, wakati LDCs nyingine 13
pengo lilikuwa asilimia 10 ya pato la jumla la taifa.
Ø Kiwango
cha utegemezi wa rasilimali kutoka nje katika kulipia uwekezaji wa ndani ya nchi
kati ya mwaka 2008 na 2010 kilikuwa 15% ya pato la jumla la taifa kwa LDCs
ambazo hazisafirishi mafuta nje.
Ø Asilimia
62 ya mauzo ya bidhaa nje kutoka LDCs 48 yalikuwa ni kutoka nchi tano tu:
Angola, Bangladesh, Equatorial Guinea, Yemen na Sudan. Ukiacha Bangladesh, nchi
zote hizi zinauza mafuta nje.
Ø Mapato
ya LDC kwa mauzo ya bidhaa nje yanategemea zaidi mauzo ya bidhaa moja (mafuta),
ambayo yanaingiza 46% ya jumla ya mapato yote yanayotokana na mauzo ya bidhaa
nje.
Ø Zaidi
ya nusu ya mauzo ya nje kutoka LDCs (54%) yalikuwa yanakwenda kwenye nchi
zinazoendelea mwaka 2011, mwelekeo unaothibitisha umuhimu wa biashara ya
kusini-kusini. China ndiyo iliyonunua bidhaa nyingi zaidi kutoka LDCs (26.4%)
ikiwazidi Jumuia ya Ulaya (20.4%) na Marekani (19%).
ZIKO WAPI NCHI MASKINI
SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa
unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo
wao ni kama ifuatavyo.
Africa (33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi,
Central African Republic, Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC),
Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau,
Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger,
Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo,
Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;
Asia (9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan,
Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste na Yemen;
Caribbean (1): Haiti;
Pacific (5): Kiribati, Samoa, Solomon Islands,
Tuvalu na Vanuatu.
Mchoro 1 – Nchi 48 za kundi la LDCs
Imetolewa na UNCTAD
Kutengeneza list ya LDCs
List ya LDCs
inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC)
la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo
(CDP).
Katika mapitio ya
hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:
1. Kigezo
cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa
(wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo
cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa
shuleni na kujua kusoma na kuandika
3. Kigezo
cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria kama mishtuko
ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na umbali.
Nchi tatu tu
zimefanikiwa kupanda daraja kutoka list ya nchi za kundi la LDCs: Botswana
Desemba 1994, Cape Verde Desemba 2007
na Maldivs Januari 2011. Samoa inategemewa kupanda daraja tarehe 1 Januari
2014.
ECOSOC ilipitisha
pendekezo la CDP kuipandisha daraja Equatiorial Guiones mwezi Julai mwaka 2009
na mwezi Julai 2012 ikakubali pendekezo la CDP kuipandisha Vanuatu. Hata hivyo
ruhusa ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa bado itahitajika ili kuzipandisha
daraja nchi hizi mbili.
No comments:
Post a Comment