ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 20, 2012

UPELELEZI WA ANAYEDAIWA KUMTESA MTOTO MBEYA WAKAMILIKA


Mtoto Aneth (3) kabla ya kukatwa mkono.
Na Mwandishi Wetu
UPELELEZI wa kesi ya mwanamke anayetuhumiwa kumnyanyasa mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto na kumlazimisha kula kinyesi chake, mjini Mbeya umekamilika.
Mtuhumiwa Wilvina Mkandala.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia Mahakama ya Mbeya kuwa upelelezi wa kesi ya mtuhumiwa Wilvina Mkandala ,24, umekamilika na akaomba tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo ambapo inadaiwa alisababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth (3) ambaye amekatwa mkono.
Alisema upande wa Jamhuri una mashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wao mahakamani hapo Novemba 22, mwaka huu kutokana na upelelezi kukamilika na akawataja kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale, dokta Paul anayemtibu mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, polisi aliyepeleleza kesi hiyo, WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao.

Mulisa akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Gilbert Ndeuruo amesema kosa alilolifanya ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo ametupwa rumande hadi Novemba 22, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. (GPL)

No comments: