ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 26, 2012

WALIOWAPIGA RISASI MAPADRI IRINGA WAANZA KUJITETEA KABLA YA WAKATI

Na Mwandishi Wetu, Iringa
WATUHUMIWA wawili kati ya saba wanaokabiliwa na kesi ya kuwapiga risasi mapadri, Angelo Burgio (60) na Herman Mallya ( 36), Jumatano ya wiki iliyopita walianza kujitetea ambapo ilibidi Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Juma Hassani anayesikiliza kesi hiyo, awaambie wasubiri muda wa kufanya hivyo ufike.

Washitakiwa walioanza kujitetea ni Alex Mgunda ambaye alidai yeye hahusiki na tukio hilo kwa kuwa siyo mkazi wa Isimani kama alivyoshitakiwa na polisi.
Naye mshitakiwa namba moja, Joseph Ngwale (30) aliiambia mahakama kuwa maelezo aliyotoa polisi aliyatoa akiwa hajitambui kwa kuwa alipokuwa kituo cha polisi alipewa mkong’oto mkali na askari hivyo kujikuta akiongea yasiyoeleweka.
Hata hivyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Juma Hassani anayesikiliza kesi hiyo aliwaambia watuhumiwa hao kuwa wakati wa kujitetea haujafika, hivyo wasubiri muda wa kufanya hivyo ukifika.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Joshua Mlagala, Bruno Mdemu, Daudi Ngwale, Erasto Ngwale na Gaituni Kitwange na kesi hiyo itatajwa tena Desemba 6 mwaka huu.

No comments: