Wanawake 517 huuawa kila mwaka nchini kwa imani za kishirikina na 24 kati ya hao ni wa kutoka Mkoa wa Singida.
Mratibu wa Kanda ya Kati wa Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopinga ukatili wa kijinsia (Mkuki), Sara Mwaga, aliyasema hayo katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.
“Taarifa za kitaifa za polisi kwa mwaka 2009/2010 zinaonyesha kuwa wanawake 517 huuawa kila mwaka kwa imani za kishirikina na 24 kati ya hawa ni wa kutoka Mkoa wa Singida,” alisema.
Mwaga alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na Tanzania Demographic Health Survey (TDHS) wa mwaka 2010 unaonyesha kuwa moja kati ya kila wanawake nchini wameshawahi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono maishani mwao.
Pia alisema utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 10 ya wanawake nchini walifanya kitendo cha kujamiana kwa mara ya kwanza kwa kulazimishwa na si kwa hiari yao.
“Utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 39 ya wanawake nchini wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo,” alisema Mwaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la AFNET.
Aidha, alisema maadhimisho ya kitaifa yatafanyika mkoani Singida kwa mwaka huu na yanaratibiwa na shirika la Msaada wa sheria (WILDAF) kwa kushirikiana na Shirika la Action Aid chini ya Mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini Mkuki.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Funguka, Komesha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na sote tuwajibike.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Gerimana Orotha, alisema bado ziko changamoto nyingi katika utekelezaji wa sheria dhidi ya ukatili wa kijinsia, ikiwemo rushwa, ukosefu wa vitendea kazi na umbali wa huduma muhimu hasa miundombinu mibovu hasa vijijini.
“Lakini ndio maana tumeruhusu wadau mbalimbali wakiwemo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuchangia juhudi hizi, na kuziba baadhi ya mapengo yaliyojitokeza,” alisema.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Ismail Kaitila, alisema matukio mengi ya ukatili wa kijinsia hutokea katika kipindi cha kiangazi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment