Advertisements

Sunday, December 9, 2012

Mtaalamu wa viungo toka India kuwasili kesho

Mtaalamu wa viungo na magoti kutoka nchini India Dk.Deodhar Shrirang anatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumatatu kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wagonjwa wenye matatizo ya aina hiyo hapa nchini.

Mtaalamu huyo kutoka hospitali ya Shalby nchini India atawafanyia uchunguzi watu wenye shida hiyo kwa siku tatu kuanzia Jumanne hadi Alhamisi wiki ijayo katika zahanati ya Regency Satellite Kliniki iliyoko Kisutu Dar es salaam.

Alisema hiyo ni fursa pekee kwa wananchi wenye matatizo hayo kwani baada ya uchunguzi watapatiwa ushauri wa kitaalamu na mtaalamu huyo kuhusu namna ya kumaliza matatizo yanayowakabili.

“Hii ni fursa nzuri kwa watanzania kuja kufanyiwa uchunguzi na mtu aliyebobea kwenye taaluma hiyo na kupata ushauri wa kitaalamu, atyafanya kazi hii kuanzia tarehe 11 hadi 13,” alisema Dk Kanabar.

Dk Kanabar alisema wagonjwa wote watakaotaka kumwona daktari huyo ni vyema wakafika hospitalini hapo wakiwa na picha za X-Ray za hivi karibuni na ripoti za madaktari walikotibiwa.

“Wagonjwa 200 tu watakaokuwa wa kwanza ndio watakaopata fursa ya kumwona mtaalamu huyo kwa hiyo watanzania wachangamkie fursa hiyo waje kupata ushauri wa kitaalamu,” alisema.

CHANZO:NIPASHE

No comments: