ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 4, 2012

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi aanza ziara Mkoa wa Katavi, Rukwa na Kigoma.


Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliejiziba uso), akisalimia na Viongozi mbalimbali wa Mkoa Mpya wa Katavi mara baada ya kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Mpanda jana mchana, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bw. Paza Mwamlima. Naibu Waziri wa Uchukuzi atakuwa na Ziara mkoani Katavi , Rukwa na Kigoma kukagua shughuli mbali mbali zinazofanywa na Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyesimama), akifafanua jambo kwa uongozi wa Mkoa wa Katavi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Naibu Waziri atakuwa na ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), pia atakagua utendaji katika stesheni ya Reli Mpanda na hatimaye kumalizia ziara yake Mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba(Mwenye Suti ya Kaki), akifafanua Jambo kwa Bw. Peter Geay(Aliyevaa flana nyekundu),alipotembelea Stesheni ya Reli Mpanda jana asubuhi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkr Charles Tizeba akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL) katika stesheni ya Mpanda, alipotembelea leo asubuhi. Naibu Waziri ameuagiza uongozi wa Shirika la Reli kuleta mapendekezo ya nyongeza ya Mishahara mapema ili Serikali iiangalie namna itakavyoweza kuwaongezea kwa mwaka ujao wa fedha.
Bw. Thomas Leopord, mmoja wapo wa wafanyabiashara akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(Hayupo pichani), wakati wa mkutano wake na Wafanyakazi wa Stesheni ya Mpanda na wafanya biashara wanaoutmia Stesheni hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(alivaya suti ya kaki), akisisitiza jambo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL)katika stesheni ya Mpanda, alipotembelea kuona namna stesheni hiyo inavyofanya kazi.

No comments: