ABIRIA mmoja amefariki papohapo huku akiwa na zaidi ya Sh13 milioni mfukoni, wengine 48 wamejeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Wakati ajali hiyo ikitokea Mbeya, Dar es Salaam watu wawili wamefariki dunia baada ya mabasi ya daladala kugongana maeneo ya Kongowe, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa magari hayo yaliyokuwa yanashindana.
Majeruhi 12 walipelekwa Hospitali za Temeke na Muhimbili kwa matibabu.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Dereva wa basi hilo, Alex Bunyinyiga alisema wakati akiendesha basi hilo, alipofika kwenye mteremko wa Inyara, mahali ambapo kuna kona kali, aliona lori lililokuwa limeegeshwa upande wa kulia wa barabara.
Bunyinyiga alisema alipolikaribia lori hilo, ghafla lilitokea gari lingine aina ya Fuso ambalo lilipita lori lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo ingesababisha kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alimtaja mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila, mkazi wa Mama John, mjini Mbeya.
Diwani alisema Lwila wakati akipatwa na ajali alikuwa na Sh13 milioni mfukoni ambazo ziliokolewa na polisi waliowahi eneo la tukio. Diwani alisema kwa sasa fedha hizo ziko salama mikononi mwa polisi na kwamba, baada ya kupatikana nduguwatakabidhiwa.
Mwananchi
1 comment:
una million 13 mfukoni halafu unapanda daladala! ama kweli ubahili mwingine too much, anyway RIP
Post a Comment