ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 17, 2013

Happy 38 birthday.Sleep on and on


DOMITIAN RUTAKYAMIRWA.ENZI YA UHAI WAKE

NAMI YALINIKUTA BY KAGEBRIANA

KUMBUKUMBU YA BABA DOMITIAN RUTAKYAMIRWA.

Shkamoo, mimi ni mtoto wa baba Domitian Rutakyamirwa, na nitaelezeya historia ya baba yangu Daddy Domi.

Kabla hajaanza kuumwa alikuwa ananipeleka shule na alikuwa anatupenda sana na alikuwa anatununulia ice cream tukitoka shule na kwenda kwenye bembea.

Tuki funga shule alikuwa anaenda kwa jirani yetu kumcheki na kumpikia chakula kwa jirani yetu, alikuwa mzee so hakuweza kupika.

Baada ya hiyo alianza kuumwa ,baada mama yangu alikua anamuliza kwa nini ana lala sana? Akasema anapenda kulala. Mama akaleta ambulance, wakamchukua baba, the ambulance hawakumcheki , baadaye alienda hospitalini kumcheki. Doctor akamwambia kwamba ana kansa ya kichwa.

Mama alikua haendi kazini kwa sababu baba alikuwa anaumwa.


Hospitali ambayo alienda ilikuwa inaitwa Howard University. Mama kila siku alikuwa anaenda hospitalini. Doctor alimwambia kwamba anapashwa kupata operation ya kichwa.

Alipata operation nne na walipashwa kutoa mfupa wa damu .

Nessi alikuwa anatengeneza mfupa wa plastiki, kesho yake asubui akafariki

Before hajafariki, alimpokea Yesu!

Siku hiyo watu wengi walikuwa wanalia sana. Nilikua najitahidi not kulia sana lakini watu wengi walikuwa wanalia sana so nikaanza kulia ,baadaye wakaacha na mimi nikaacha.

Wakajiandaa kutoka, kesho inayofuata tukafanya maziko ilivyomalizi ka mama yangu alisema kesho yake ataondoka kwenda Tanzania kumzika Daddy Domitian,

Mimi na wadogo zangu tulienda kwa mama’s friend hapa Washington D.C.

Mama, mimi na wadogo zangu tulikua tunampenda sana kabla hajakata roho na Baba Domitian alikuwa anatupenda sisi pia lakini aliondoka akatuacha sisi.

Kabla hajafariki alikuwa anataka kununua gari yake ambayo alikuwa anapenda sana lakini aliondoka na mama ajaribu kupata hela so aende kununua a LAND ROVER for daddy so baba yangu daddy afurahi sana wakati yuko mbinguni.

Siku Daddy alipofariki nilisikitika sana. Siku zote nilikuwa namkumbuka. Na siku mmoja nilivokua shuleni rafiki yangu aliniuliza kwanini baba yangu haji shuleni kun chua only mama yangu? Mimi nika mwambia kwamba baba alikufa kwa sababu ya kansa, rafiki yangu hajacheka wala kushangaa pia, kwa sababu aliniambia kwamba na yeye mama yake alikufa pia kwasabu ya kansa pia.

Rafiki yangu akasema pole na mimi nili mwambia pole pia. Mama yangu akani ambia kwamba watu wengi wana kufa sana so unatakiwa uwe unavumilia sana, akaniambia kwamba maisha ni magumu sana, nikaelewa. Sasa hivi ni mimi, Mama, na wadogo zangu, Bryan, Bryton.

Rafiki zetu Nicole na Michelle wanakujaga ijumaa na wanakaa mpaka jumapili. Tunafurahi pamoja

Mimi nimemmisi sana Daddy Domi. Siku ya christmasi nilimkumbuka baba yangu, nilitamani baba yangu angekua kwenye sherehe ya christmasi na sisi. Wadogo zangu wamemmisi sana na mama yangu alikua anampenda sana lakini mungu alimpenda zaidi.

Natamani ujumbe wa barua hii ukufikie uko mbinguni ulipo kutoka kwangu mimi binti yako ninaye kukumbuka sana.

Natamani ungekuwepo kwa Birthday yako ila jua tunakupenda na tutakukumbuka daima.

Mama anajitahidi kututunza nasi tunamsaidia kama tulivyo kupromisi hospitalini,George Washington Hospital.

Asante kwa kutuombea kwa Mungu uwe na amani kabisa .Kanjunju anaenda shule sasa. Na asubuhi akiamka akiwa ana usingizi analia anamwambia mama “take me to daddy Dommy” mama anamwambia “He went to heaven to pray for us”

Mama amenunua keki yako ya Birthday leo.

Sleep on and on my lovely daddy Domitian.January 17th 1975 – June 18th 2012




FROM:KAGEBRIANA

8 comments:

Anonymous said...

Pole sana Briana Mungu akutie nguvu..kwa kweli u mdogo sana lkn maneno uliyozungumza yamenifanya nipate funzo kubwa kwako,na hii inatokana na mama yako kutoacha kukupeleka kanisani wewe na wadogo zako,naamini siku moja utamuona baba yako siku ile parapanda itakapolia,endelea kuwa na moyo wa ujasiri na uvumilivu na usiache kumkumbuka baba yako kila inapofika birthday yake.MUNGU WA REHEMA AKUTANGULIE KWA KILA JAMBO UTAKALOFANYA.AMEN!!! ....AUNT LILIAN

Anonymous said...

Pole sana Binti Briana.Nafurahi kwa good memories za Dommy.Sikupata kumjua ila nilisikia kuhusu kuugua kwake.Stay strong kwa mama yako na wadogo zako.Mngu awabariki sana. Anita J.M

Rachel Siwa said...

Pole sana Binti....MUNGU azidi kuwapa nguvu na Uvumilivu.

mussa linga said...

OMG , sikutegemea kama utakumbuka haya yote, wewe ni motto mzuri sana kwa maneno mazuri kwa baba yako ambaye ni rafiki yangu,, mungu amuweke mahali pema peponi, na pia akupe uwezo mara mbili yahapo , mpe Hi kabuju.mimi anko Mussa.

Anonymous said...

Poleni sana Mungu awatie Nguvu na awabariki.

Anonymous said...


Binti huyu kweli ameongea maneno yenye kugusa sana, shukrani kwa "tribute" kwa baba yako mpendwa.

In New Haven,CT.

Anonymous said...

Poleni sana lakini Mungu ndiye ajuaye kwa hayo yote mliyoongea, mimi ni Leonce Domitian Rutakyamirwa ni mtoto wa Marehemu sikujua kama kuna wadogo zangu huko Marekani mbona hamjaja kumzika baba yetu Tanzania?

Anonymous said...

Mungu atusaidie tuweze kumuenzi Domitian kwa yaliyo na ukweli ndani yake na tujue kwamba yuko mbele za haki tusimuongezee mizigom poleni sana watoto kwa kumkumbuka baba mlezi aliwalea kwa upendo sana.