ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 25, 2013

Hospitali ya rufaa Mbeya yashitukia ubadhilifu na rushwa

Katibu wa Hospitali Aisha Mtanda akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa hospitali ya rufaa Mbeya
Mwenyekiti wa kamati ya sherehe Christopher Mwakubombaki moja wa waandaaji wa bonanza hilo
Mratibu wa Bonanza hilo kutoka Kampuni ya Lifetime Venance Matinya 
Meneja wa kampuni hiyo ya LifeTime Entertainment, Emmanuel Madafa, 



KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika taasisi za Serikali, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya imeamua kuandaa Bonanza kubwa la michezo kwa ajili ya kukutana na wananchi ili kukemea vitendo hivyo.


Aidha hali hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kuingiwa na kashfa kwa baadhi ya watumishi wake wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya Kupokea Rushwa kutoka kwa wagonjwa hususani katika kitengo cha Mifupa.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, katibu wa Hospitali hiyo, Aisha Mtanda alisema kuwa bonanza hilo ambalo litabeba ujumbe usemao ‘Huduma bora bila rushwa inawezekana, kemea vitendo vya vya rushwa, tuungane kutokemeza limeandaliwa na Uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya LifeTime Entertainment & Marketing Ltd na kwamba bonanza hili litafanyika siku ya Jumamosi(Januari 26, mawaka huu).
Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kufanya hafla fupi kwa watumsihi wa Hospitali hiyo kwa kuaga mwaka wa 2012 na kuukalibisha mwaka mpya wa 2013, ambalo pia litafanyikia katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA)tawi la Mbeya.
“Uongozi wa Hospitali tunakusudia kufanya bonanza litakalowakutanisha watumishi wa serikali pamoja na taasisi mbalimbali siku ya Jumamosi Katika bonanza letu litakuwa na ujumbe wa kukemea vitendo vya rushwa vinavyoonekana kushamiri katika sekta mbalimbali,” alisema katibu huyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza hilo kutoka Kampuni ya Lifetime Venance Matinya alisema katika Bonanza hilo kutakuwa na michezo mbali mbali kama vile mpia wa miguu, mpira wa pete, Netboli, Basketi boli, Voleboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia,kukuna nazi na mashindano ya kula.
Aliongeza kuwa taasisi zinazotarajia kushiriki ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Halmashauri ya Jiji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Madiwani wa Halmashauri wa Jiji, Kampuni ya Bia (TBL), Hospitali ya Rufaa na kitengo cha Benki ya damu salama.
Naye meneja wa kampuni hiyo ya LifeTime Entertainment, Emmanuel Madafa, alisema kuwa katika mabonanza hayo ni sehemu pekee ya kukutana kwa watumishi mbalimbali na wananchi ili kuweza kuambizana ukweli kuhusu adii mbaya wa rushwa.
Alisema kuwa vitendo vya rushwa haviwezi kukomeshwa endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa kuambizana ukweli, kwani wananchi muda mwingine wanaweza wakawa wanashawishiwa kutoa rushwa kutoka kwa watumishi bila ya kujua haki zao za msingi na wasijue wapi wanaweza kwenda kutoa malalamiko yao.
“kwenye mabonanza kama haya ni sehemu pekee ya kuweza kukutana wananchi pamoja na watumishi wa Serikali na taasisi mbalimbali ili kuweza kuambizana ukweli kuhusu adui rushwa kwani hawa watu wawili ndiyo wahusika wakuu kwamaana ya mpkeaji na mtoaji,” alisema Madafa.
Hivi karibuni Mmoja wa watumishi wa Hospitali hiyo wa kitengo cha mifupa alikamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa anahitaji kupatiwa huduma ya upasauaji.

No comments: