ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 25, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MKESHA WA MAULID MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkesha wa sherehe za Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W). 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumin wa dini ya Kiislamu, katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013. Kushoto kwake ni ,Sheikh Mohamed Ismail. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W.).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mohamed Ismail, wakati akiondoka kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, baada ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Sheikh Mohamed Ismail, wakati alipokuwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, kwenye sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu zake za mkesha wa sherehe za Maulid, ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), wakati wa sherehe hizo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na waumin wa dini ya kiislamu wakijumuika kwa pamoja katika sherehe za mkesha wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika jana usiku katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments: