ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 16, 2013

KERO YA WATUMIAJI WA ZANTEL

Kwa zaidi ya wiki sasa watumiaji wa simu za mkononi ya ZANTEL wamekuwa wakisumbuka kutoka na huduma zao lakini jambo la kushangaza licha ya kuwa ZANTEL kuwa ni mahodari kuwatumia ujumbe wateja wao lakini katika hili wameshindwa kuwatumia au kuwaomba radhi wateja wao kwa tatizo hilo au usumbufu wanaoupata kutokana na huduma hiyo ya kutuma ujumbe (sms-msg) huwa hazipatikani na unapotuma amma hazendi kabisa au zinachukua muda mrefu kumfikia unayemtumia ni kwa nini? 
Nadhani panapotokea tatizo serious kama hili Kampuni isisite kuomba radhi kwa wateja wake lakini pia kuwaeleza kwamba tatizo hilo ni la muda fulani kwa sababu kuendelea kukaa kimya kuonaonesha kutowajali wateja wenu. Ahsanteni. mimi nimesumbuka sana jee wewe umeshawahi kupata usumbufu huu na nini kifanyike kwa Kampuni zaidi ya kuomba radhi?

No comments: