Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari nchini China alipofanya ziara juzi.Picha na AFPAFP
China. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, amewasili nchini China, katika juhudi za kuishawishi nchi hiyo kuishinikiza Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa nyuklia
Akiwa nchini humo Kerry alisema China na Marekani wana lengo moja la kusuluhisha mzozo wa kinyuklia wa rasi ya korea na kuitaka Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo ya kimataifa.
Kerry alifanya mazungumzo na Rais Park Geun-Hye na kuahidi msaada wa Marekani katika mipango yake ya kuanzisha nia ya kufanya mazungumzo na majirani zake ili kutuliza hali ya wasiwasi inayoongezeka.
Katika mkutano wake na maofisa wa chama tawala uliofanyika jana, Rais Park amesema Korea Kusini inapaswa kukutana na Korea Kaskazini, ili kusikiliza nchi hiyo.
Wakati Kerry akiionya Korea Kaskazini kuachana na mpango wa kufanya jaribio la kombora, na kwamba nchi hiyo haiwezi kukubalika kama taifa lenye nguvu ya nyuklia, kufanya hivyo nchi hiyo itakuwa imefanya kosa kubwa.
Kerry alisema Rais Park alichaguliwa kwa misingi tofauti ukiwemo uwezekano wa kuleta amani na kwamba Marekani inaheshimu hali hiyo.
Alisema wamejiandaa kufanya kazi kwa imani kwamba uhusiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini utaimarika haraka.
Katika ishara nyingine ya kuonyesha kuwa Marekani ina matumaini ya kumaliza mvutano uliopo, Kerry hakutembelea kijiji cha makubaliano ya kusitisha mapigano cha Panmunjom, kituo ambacho kwa kawaida viongozi wa kigeni hukitembelea, pindi wanapozuru Seoul.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment