ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 22, 2013

RUFAA KESI YA ZOMBE YASOGEZWA MBELE, LEMA APETA-GPL

Lema akipongezana na Mwanasheria wa Serikali Alute Akida mara baada jopo la majaji kutoa uamuzi. 
Wandishi wa habari wakizungumza na Wakili Tundu Lissu aliyekuwa akimtetea Lema.
Lema akizungumza na wana habari mara baada ya rufaa kutupwa.
Mbunge Godbless Lema akionyesha ishara ya vidole inayotumika na chama chake wakati akitoka mahakamani.

RUFAA ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Abdallah Zombe na askari wenzake wanane ya mauaji ya wafanyabiashara wawili na dereva taksi mmoja iliyokuwa ianze kusikilizwa leo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania imeahirishwa.
Kesi hiyo haikusomwa mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa hati ya mashitaka ina makosa.
Hata hivyo, haikuelezwa lini shauri hilo litasikilizwa mahakamani hapo japokuwa Zombe na wenzake walikuwepo katika mahakama hiyo.
Wakati huohuo, rufaa ya kesi ya Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema imetupiliwa mbali na mahakama kumtangaza mbunge huyo kuwa ni halali.
Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Rufaa Tanzania ambao ni Engili Kileo, Salum Massati na Benard Luanda kwa pamoja wametupilia madai ya rufaa hiyo.

No comments: