Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari wa Chama cha Waandishi wa Umoja wa Mataifa siku ya jumatano, katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alieleza imani yake kubwa kwa Brigedi Maalum itakayopelekwa Mashariki mwa DRC kwamba itatoa mchango mkubwa sana katika uimarishaji wa amani na usalama na hivyo haikua haki kuanza kuihukumu kabla hata haijafika eneo la jukumu. Mwezi uliopita Baraza Kuu la Usalama lilipitisha Azimio ambalo pamoja na mambo mengine liliridhia kupelekwa kwa Brigedi hiyo maalum na imeipa Brigedi dhamana na uwezo pale itakapolazimika kutumia nguvu kuyadhibiti makundi ya wanamgambo wenye silaha ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiendelea kulifanya eneo hilo kutokuwa na amani na usalama wa kudumu.
Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon, amesema si haki
kuanza kuihukumu na kutupia lawama
Brigedi Maalum (Intervention Brigade )inayotarajiwa
kupelekwa Mashariki ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) hata kabla Brigedi hiyo haijafika eneo lake la jukumu.
Kauli hiyo ya Katibu Mkuu,
imefuatia swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi kutoka
Chama cha Waandishi wa Umoja wa Mataifa alipokutana nao siku ya jumatano, ambapo alizungumzi masuala mbalimbali muhimu yanayoendelea hivi sasa
duniani katika nyanja za usalama,
uchumi na maendeleo.
Katika swali lake,
mwadishi huyo aliuliza kuwa, baada ya
Baraza Kuu la Usalama, kupitisha Azimio ambalo limeridhia kupelekwa kwa
Brigedi maalum kumejitokeza maoni tofauti kutoka kwa makundi mbalimbali ya jamii, yakiwamo ya
wanawake.
Maoni hayo ni pamoja na kuwa ,
upelekaji wa brigedi hiyo maalum kunaweza kuchangia uzotoraji zaidi wa amani na usalama na hivyo kuhatarisha zaidi haki za binadamu zikiwamo za wanawake. Na nini
yalikuwa maoni yake (Katibu Mkuu ) kuhusu
brigedi hiyo na mstakabali wa
haki za wanawake.
Akijibu swali hilo, Ban Ki Moon, alisema. “ Azimio
lililopitishwa na Baraza Kuu la
Usalama mwezi uliopita kuhusu upelekeaji wa brigedi mpya kwanza ,ni
Dhana mpya lakini pili huu ulikuwa uamuzi muhimu sana. Si haki kwa
kweli, kuanza kuihukumu na kuitupia lawama brigedi hiyo hataka
kabla haijafika DRC”.
Na kuongeza. “Tuko katika
maandalizi makubwa ya kufanikisha upelekaji wa brigedi hii maalum . Ni
matumaini yangu kwamba brigedi itatoa mchango mkubwa sana katika uimarishaji wa amani na usalama katika DRC”.
Akaongeza kwa kusema upelekaji wa brigedi
hiyo unaimarisha uhakika wa
hatimaye kupatikana amani, usalama
na ulinzi wa raia, pamoja na kulinda haki za binadamu zikiwamo
za wanawake.
Akafafanua zaidi kwamba,
mwishoni mwa Mwezi ujao ( Mei)anatarajia kwenda kuhudhuria mkutano wa Kilele wa
wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa
Afrika ( AU).
Na kwamba wakati wa mkutano huo atakutana
na kufanya mazungumzo na viongozi 11 na
wadhamini wanne ambao mwezi February
2013 huko Addis Ababa, Ethiopia, walitia saini
Mpango mpana wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa wa amani, usalama na ushirikiwano wa maendeleo katika DRC na eneo
la Maziwa Maku
Itakumbukwa kwamba mwezi
Marchi mwaka huu, Baraza Kuu la Usalama
katika tukio la kihistoria lililoambatana na maamuzi magumu lilipitisha kwa
kauli moja azimio namba 2098 ( 2013) ambalo pamoja mambo mengine, liliidhinisha
upelekaji wa Brigedi Mpya katika DRC.
Brigedi maalum itaundwa na wanajeshi 3,069 kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini, na Malawi itakakuwa na uwezo, pale itakapolazimika, wa kuyakabili,
kuyadhibiti na kupokonya silaha makundi ya wana mgambo yenye silaha katika nchi
hiyo hususani katika eneo la Mashariki.
No comments:
Post a Comment