Wachezaji wa timu ya Far Rabat, wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo tayari kuwakabili wapinzani wao, Azam Fc katika mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya pili, unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, jumamosi ya wiki hii.
Baadhi ya viongozi wa timu hiyo wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili leo mchana. Picha na Lenzi ya Michezo.
“Timu yetu ni nzuri na Azam pia ni wazuri kwani wana wachezaji waliopo kwenye timu ya taifa hivyo tutahakikisha tunafunga mabao 2-0 ili iwe rahisi wakija nyumbani”, alisema Younes.
Wachezaji wa Far Rabat ambao wapo kwenye timu ya Taifa ya Morocco ni Hammal Younes, Achchakir Abderrahim, Bellakhdar Younes, Saidi Salaheddine, Aqqal Salaheddine na Youssef Kaddior.
Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara wa watu 31 na umefikia kwenye hoteli ya Saphire iliyoko Kariakoo.
No comments:
Post a Comment