Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya timu ya JKT Oljoro
"sita, saba, nane,tisa, kumi , kumi na sita, kumi na nane, ishirini na tano, ishirini na sita"
Hivyo ndivyo washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Young Africans Sports Club leo walivyokua wakihesabu pasi murua (sambusa) wakati mchezo ukiendelea huku wakicheza na kufurahi kwa makofi, ambapo timu ya Yanga ilikua inaongoza kwa mabao 3-0, katika mchezo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhid ya timu ya JKT Oljoro mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom baada kufikisha point 52 na mabao 40 ya kufunga, pointi 6 mbele ya timu inayoshika nafasi ya pili Azam Fc yenye pointi 46 huku timu zote zikiwa na michezo sawa 22.
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 5 ya mchzo kupitia kwa mlinzi wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' aliipatia bao la kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona iliyokuw aimepigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Watoto wa jangwani walionyesha kuwa wamedhamiria kupata ushindi mnono leo kwani waliweza kucheza soka safi na la kuvutia huku Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wakikosa mabao ya wazi ndani ya dakika 15 za kwanza.
Kiungo chipukizi mwenye kasi Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao pili dakika ya 19 ya mchezo kufuatia kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya JKT Olljoro na Msuva kumchambua kwa umaridadi mlinda mlango wa JKT Oljoro na kuhesabu bao la pili kwa timu ya Yanga.
Yanga iliendelea kulishambulia lango la JKT Oljoro muda wote wa mchezo na mashuti ya washambuliaji wa Yanga yalimfanya mlinda mlnago huyo kutibiwa mara kwa mara kwa kukoa michomo ya washambuliaji wa Yanga.
Dakka ya 43, mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao la tatu kufuatia mpira aliopenyezewa na kiungo Frank Domayo na Kiiza kuwatoka walinzi wa JKT Oljoro na kuiandikia Yanga bao la tatu.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambapo waliingia Nizar Khalfani na Said Bahanuzi kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu aliyeumia na Simon Msuva mabadiliko yaliongeza ufundi zaidi na kuutalawa mchezo kwa kipidndi chote.
Said Bahanuzi alifanyiwa madhambi wakati akiwa ndani ya eneo la hatari akijandaa kumchambua mlinda mlango wa JKT Oljoro lakini mwamuzi wa mchezo na mwamuzi wa pembeni wake hawakujali na kuendelea na mchezo.
Zikiwa zimebakia dakika tano kabla yakumalizika kwa mchezo, kiungo mshambuliaji Nizar Khalfani alikosa bao la wazi kufuatia shuti lake kuokolewa na mlinda mlango wake ambapo mpira huo ulipigwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.
Wachezaji wa Young Africans wakimpongeza Saimon Msuva mara baada ya kufunga bao la kwanza
Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema anashukuru timu yake kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza timu yangu ilicheza kwa nguvu na kupata mabao ya mapema hali iliyoplekea kipindi cha pili kucheza soka la burudani.
Timu imekua na mabadiliko makubwa sana kiuchezaji na leo timu imecheza soka safi la burudani lililoambatana na ushindi, hii ni zawadi kwa washabiki, wapenzi wa soka na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa njia ya kutwaa ubingwa kwa sasa ni nyeupe.
Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Mgambo Shooting siku ya jumatano mjini Tanga ambapo timu itasafiri siku ya jumatatu tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili kuendelea kujiweka vizuri katika nafasi ya kutwaa Ubingwa kabla ya kumalizika kwa msimu.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Shadrack Nsajigwa, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani , 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu/Said Bahanuzi,10.Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima
No comments:
Post a Comment