Afisa Masoko wa PSPF Bi. Hawa Kikeke akitoa maelezo kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal kwenye maonyesho ya 8 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Diamond Jubelee Dar es Salaam. Alifafanua kwamba sasahivi sheria inaruhusu wafanyakazi kujichagulia wenyewe Mfuko wanaopenda kujiunga nao bila kuchaguliwa na Mwajiri pindi tu wanapopata hajira mpya.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Ndugu Ntimi Mwakajila akiwaelezea wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko ikiwemo mpango wa kuchangia kwa hiari.
Mhandisi Ujenzi mwandamizi Ally Shanjirwa na Afisa Mwandamizi TEHAMA Mariam Saleh wakisikiliza maoni ya mteja aliyetembelea banda la PSPF kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.
Mhandisi Ujenzi mwandamizi Ally Shanjirwa akielezea kuhusu nyumba zilizojengwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya kukopesha wanachama wake. Nyumba hizo zimekwisha jengwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Morogoro, Mtwara na Tabora. Lakini mchakato wa ujenzi huo unaendelea katika kila mkoa Tanzania. Nyumba hizo zinakopeshwa kwa wanachama kwa marejesho ya kila mwezi kwa muda wa miaka 25. Mteja huyo alitembelea banda la PSPF kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandalasi Mlimani City Dar es Salaam
Afisa Mwandamizi Uendeshaji Bi. Sophia Mbilikira akielezea aina mbalimbali za Mafao yatolewayo na Mfuko wa PSPF pamoja na mikopo ya nyumba. Afisa huyo alisema sasahivi sheria inaruhusu mtu kuendeleza michango yake hata kama akiacha kazi kutoka kwa mwajiri wake alipoanzia kazi na kwenda kwa mwajiri mwengine bila kupoteza uanachama wake. Aliyasema hayo kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment