Ni wazi na dhahiri kabisa kesi iliofunguliwa mahakamani dhidi ya Lady JayDee haina maana yoyote isipokuwa ni hofu ya mafisadi wa muziki nchini (Kusaga na Ruge) kwa kuwa waraka wa pili ulikuwa utoke tar 15 may na mwingine tar 17 may mwaka huu wa 2013.
Hapa la kujiuliza ni juu ya interview ya Rugen a kinachoendelea sasa,eti suala limefika mahakamani,kweli Kusaga na Ruge mmeweza kuthibitisha nyie ni mafisadi na mnamuaibisha Rais Kikwete ambaye nina uhakika anajua kuwa nyie ndio kikwazo kikubwa na hata Bungeni alishawahi kuzungumza kuwa alitoa studio na pango kumbe tatizo sio hilo,tujiulize wote kuna nini wanachoficha hadi kumtafutia kesi raia mwema asie na hatia?
Tena anaejitafutia rizki ambayo wao wanapigana nayo kwa kumkandamiza?
Huku wakitumia mabavu wakilindwa na baadhi ya viongozi wa serikali na waandishi ambao majina yao mtayapata kupitia nyaraka zinazokuja (zipo 88) na huu ndio wa kwanza.
Nimesikitika sana na njia pekee ya kuufahamisha umma juu ya ufisadi huu wa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga ni kuyaanika yote ambayo jamii na Viongozi wa Serikali kama mlikuwa hamjui sasa ndio wakati muafaka wa kuwajua watu hawa ambao kila kukicha ni kuimarisha ufisadi wao na kujipendekeza kwa Viongozi sambamba na watoto wao (mtajua mpaka majina yao)
Naanza kupatwa na wasiwasi nikijiuliza, endapo Lady JD angekuwa amegombana na msanii mwenzake mkubwa kama Prof Jay, Ray C au Juma Nature wanasiasa wangeingilia kati? Ni wazi wasingesogea kwa kuwa hakuna maslahi zaidi ya kuingilia mgogoro huu ambao hawataki jamii ijue maovu yao.
Napatwa mashaka jinsi wanasiasa wanavyolivalia njunga jambo binafsi
Kama hili na kulifanya ni la kiserikali basi tafuteni chanzo cha tatizo mjue ni sehemu gani sahihi ya kuanza kutatua kilichopo na sio kukimbilia kuunda vikao ambavyo naamini vimeshaitishwa vingi sana lakini hakuna kilichosaidia.
Wanasiasa badala ya kutafuta sababu zinazofanya wasanii wanalalamika mnakimbilia kutatua mgogoro wa Ruge na JD ili kusuluhisha mambo yasiendelee kuongelewa jamii ijue uovu wa mafisadi hawa.
Haitasaidia kwa sababu wanaojua maovu ya hawa mafisadi Rugen na Kusaga ni wasanii wengi wakubwa na watu wengine binafsi (kumbukeni waraka zipo 88)
Vijana mnaowategemea katika kampeni zenu na mnawaita Taifa la kesho, lakini mnakubali waendelee kukandamizwa na kunyanyasika huku wakizidi kuwaneemesha kina Ruge na Kusaga.
Tatizo mnalijua kaeni na wasanii wote wawaelezee matatizo yao, msikae na wasanii ambao wanaamrishwa na kina Ruge. Sikilizeni kilio cha wasanii wengine pia na itafutwe njia ya kupata maoni ya kila mmoja na kuachana na watu wengine ambao wanaendesha mtandao wa ufisadi chini ya kivuli cha Ruge (Said Fella na Babu Tale) ambao mtapata kujua kila kitu kuhusu ufisadi wao na kinachoendelea (kumbuka waraka zipo 88)
Ruge Mutahaba amekuwa ni tatizo na janga la Kitaifa katika tasnia ya muziki kwa ujumla, amekuwa akiwagawa wasanii kwa kutumia redio Clouds kwa vitisho vya kutopigiwa nyimbo, au kwa danganyio la kufanyiwa promotion mpaka kwenye magazeti endapo tu utakuwa chini ya bawa lake.
Wasanii wamekuwa hawalipwi vizuri ili waendelee kumtegemea fisadi huyu.
Kwani wasanii wote wangekuwa na kipato cha kuweza kusimama imara leo hii kauli kama ya Lady JD ingezungumzwa karibu na kila mwanabongoflava.
Fred Kavishe (fisadi mwingine) ambae anasimamia Kili music awards yuko bega kwa bega na Ruge kudanganya wananchi nani ni bora katika tuzo hizo ili kulinda maslahi yao binafsi.
Na wao huchagua wale wasanii ambao hawana sauti za kudai haki yao ili wawatumie kadri wanavyotaka.Tuzo za Kili ni uozo mtupu.Imefikia wakati basata itoe vibali kwa wadau wengine wa muziki (nako kuna ufisadi)wasio na interest binafsi na wasanii wao, kuendesha hizi shughuli ili kukuza muziki.Kutokuwepo na tuzo zingine kunasababisha ionekane kuwa basata nao wamo kwenye mgao wa mabepari hao wanaoua sanaa ya Tanzania
JINSI RUGE NA KUSAGA WANAVYOTAWALA
Njia anayoitumia Ruge na Kusaga iko wazi, wao wana redio na hapo hapo wana wasanii wao.Hivyo promotion inabidi wafanyie wasanii wao ambao ni waoga ili waweze kuwatumia bila wasanii hao kufanya fyoko fyoko.
Wasanii wengine ambao sio chini ya Clouds kwa kuwa hawana jinsi nyingine ya kupata hela inabidi wainyenyekee Clouds wakiamini ndio njia pekee ya kuwapatia vipato
Huku wakisubiri show moja ya fiesta ya kila mwaka.
Huko katika fiesta kuna wengine wanalipwa mpaka laki tatu na bado katika hiyo ili upangwe kwenye list ya kupanda jukwaani B12 nae lazima akate laki moja yake.
Hapo msanii anabakiwa na nini akirudi nyumbani?
Hivi laki tatu ni nini kwa maisha ya msanii?
Njia pekee ya kuwatawala ni kuwafanya waendelee kuwa maskini.
Leo hii mtangazaji wa redio ana sauti kuliko msanii.
Kwanini redio zingine hazilaumiwi? Ni kwa sababu hazijihusishi moja kwa moja na wasanii.Hilo ni kosa kubwa sana linalofanywa na Clouds au pengine ndio mtazamo wao walioamua kuufuata kwa sababu wanaamini Serikali ipo mikononi mwao.
Maisha na ajira za watoto wa watu ambao wengi hawajasoma wanategemea vipaji, mnayakatili bila huruma
Mwisho tumuombee Lady JD Mahakama imruhusu azungumze yote, kila mtu anataka kusikia sio siri Clouds, Ruge na Kusaga ni nyonya damu.
Mahakama itambue kuwa wanaojua maovu ya Rugen a Kusaga sio Lady JayDee pekee ni wengi mno na kama njia ya kukimbilia mahakamani ndio wameichagua basi ongezeni mahakama kwa kuwa tupo wengi tutakuja kuyaongea kuhusu mafisadi hawa wa Clouds (siku hizi wanaitwa wafu)
Hela ina nguvu hata palipo na haki, JD hajatukana matusi na amekuwa makini katika kutoa kauli zake sasa anashitakiwa kwa kosa gani? Anashitakiwa kwa kudai haki yake. Anaconda wewe songa na sisi tunakuja kizimbani na sasa ndio TANZANIA itawajua Rugen a Kusaga ni kina nani na walianzia wapi,walikuwa wapi,wako wapi na nani wanaoshirikiana nao
1 comment:
Daah jmn huruma sana pole sana malkia wa Bongo Flava Mwenyezi Mungu atakusimamia na kukupa haki zako...
tupo pamoja
Post a Comment