Khadija Kopa akilia kwa uchungu hata kushindwa kutembea mwenyewe.
Dah sina hata la kusema. Pole sana mama Mwenyezi Mungu akutie Nguvu katika kipindi hiki kigumu
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa. Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana. Picha kwa hisani ya zeddyblog
3 comments:
ina lillahi waina illahim rajiun usiliye sana hivyo bi khadija kopa nafahamu fika unauchungu na kuondokewa na mumeo kipenzi lakini usiliye sana hivyo kazi ya mungu haina makosa cha kufanya kila ukisikia uchungu muombe kwa Allah ampe makazi mema na huko kaburini aweze kuyajibu maswala vizuri najua si mchezo na unchungu unao lakini jaribu na utaweza ushinde moyo wako pika konde
pole sana bi khadija kopa inana lillah waina illahim rajiun sote tutapita njia hiyo hiyo hakuna atakaye baki hapa duniani wakati ukifika hata sekunde mmoja huwezi kusubiri kiumbe unaondoa
tumuombea dua kwa sana pamoja na omary na pole sana bi khadija kopa
mdau mbaya nazipenda sana nyimbo zako
yule yule mdau wa NY
JE AMEKUFA NA UGONJWA GANI
POLE SANA MAMAA NDO KAZI YA MUNGU WOTE TUNAPITA NJIA HAPA DUNIANI SI PETU
INNA LILLAHI WAINA ILLAHIM RAJIUN
wabongo bwana hata imani hatuna ukitazama vizuri picha hii utaona kuna mheshimiwa mmoja anacheke utadhani yeye ataishi milele hapa duniani hata huruma hana angekuwa jamaa yake amekufa tungemuona kama angekenua mimeno yake mibaya kama hivyo shame on you na usidhani kwamba uko juu ya ardhi hii kwamba hakuna siku utafukiwa
Post a Comment