ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

VIJIMAMBO KURUSHA LIVE MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI

TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI NA SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO ITARUSHWA LIVE JUMAMOSI JULY 6, 2013 KUANZIA 4:00 ASUBUHI(10:00AM ET, 9:00AM CT, 7:00AM PT, 3:00PM UK TIME 5:00 PM TZA TIME)KWA KUANGALAI LIVE BOFYA HAPA

Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusherehekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha la kiswahili. Tamasha hili ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakayokuwepo ni Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo wa mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani ambao ni Shilole na Masanja Mkandamizaji wakishirikiana na wa hapa Marekani yote hayo ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

HOTEL KWA WAGENI 
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites 
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Address ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843

Hotel za jirani na hapa ni
Hampton Inn
9421 Largo Dr West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 499 4600

Extended Stay American
9401 Largo Drive West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 3339139

Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900

Muda wa watoto ni kati ya 10:00 am - 5:00 pm:
Kuanzia 7:00 pm- 3:00 am ni kwa watu wazima tu.

MAVAZI 
10:00 am - 5:00 pm Vazi la Kitanzania
7:00 pm - 3:00 am Vazi lolote lakini uwe umependeza

BURUDANI ZOTE NI KATI YA 10:00 AM - 5:00 PM
USIKU NI CHAKULA NA MUZIKI WA DISKO TU.

Chakula cha mchana Kuanzia kifungua kinywa na vinywaji  vitauzwa muda wote Dinner peke yake ndio itakayokua Free.

Tafadhali zingatia muda. Rais Mustahafu Ali Hassan Mwinyi ataingia ukumbini 10:30 am(saa 4:30 asubuhi)

KARIBU

4 comments:

yoo said...

RUKSAAAAAAAAAAAAAA

Anonymous said...

Na dinner kinywaji bure au kitauzwa?tueleweshe bwana

Catherine M Mock said...

All the best

Unknown said...

Udumu utamaduni WA mtanzania