ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 13, 2013

MTANZANIA ALIEFUNGWA UKO ANGOLA ATIRIRIKA KWA HAYA

Baadhi ya ndugu na marafiki wa Mtanzania aliehukumiwa kifungo cha miaka nane nchini Angola baada ya kupatikana na dawa za kulevya alizokua akizisafirisha kwenda Afrika Kusini, wamepaza sauti kuomba msaada wa Serikali ili ndugu yao aje kufungiwa gerezani Tanzania.

Khaleed Bin Abad amesema huyu Mtanzania aliondoka South Afrika na kwenda kufata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukua ila wakati anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.

Kwa kipindi chote hicho huyu jamaa amekua akishikiliwa Angola bila kujua hatma yake na hata kushindwa kukutana na balozi wa Tanzania Angola lakini wiki mbili zilizopita ndio amehukumiwa kifungo cha miaka 8.

Ombi lililoambatana na ndugu hawa kupaza sauti, ni kuiomba serikali kusaidia mtu huyu kukutana na balozi wa huko ili utaratibu wa kuja kufungwa Tanzania ujulikane.

Mara nyingi Mtanzania huyu amekua akituma msg kwa kutumia simu za watu wengine aliokutana nao gerezani.

8 comments:

Anonymous said...

Naomba afungwe huko huko, hata kama ni shida kiasi gani....si alitafuta mwenyewe. Mnataka serikali imsaidie ili iweje? alikutwa na madawa ya kulevya ambayo nchi zingine angeuawa/angenyongwa. Anataka aje afungwe tz ili ahonge akae nje? No haikubaliki...anatakiwa afungwe zaidi ikibidi serikali iombe aongezewe muda wa kifungo. Hatuwezi kutajwa tajwa kama nchi inayohusika sana na madawa kwa ajili ya wajinga wachache

Anonymous said...

Mdau hapo Juu uko ryt, naona sasahivi ndio mambo ya madawa yanafunguka hapa kwetu kwa wanaotumia na wanaouza madawa hayo, hii ni aibu kwa watu wanaona ni ujanja kuuza madawa, millions of watu imepotea kwa hii madawa , ndugu msijisumbue Kumtoa hata Kama angekua ndugu yangu nisingejali kabisa ni muuaji mkubwa mkimtoa mtajuta,ishia huko huko Angola wakukomeshe hufai kwenye jamii .

Anonymous said...

Hahahaha wewe anonymous wa kwanza umeniacha hoi kweli kweli ungekewa judge wewe watu wangechezea mvua za nguvu, lakini umezungumza ukweli mtupu,anyway ndo vijana wetu hao wanataka utajiri wa haraka haraka.

Anonymous said...

hehehehehehe Naomba afungwe huko huko Angala tena asirudishwe popote pale....aliye mtuma auze madawa ya kulevya nani? sasa anataka kutubabaisha hapa anasema Nomar angelijua habari ya Nomar kabla hajabeba hayo madawa ya kulevya. wanafunza hawana madawati wanaketi chini, walimu mshahara mdogo, umeme hautoshi kabisa na vitu vingine vya maana na muhimu zaidi yeye anataka serekali ihangaike kumchomoa jela ya Angola??? NO he needs to be locked up in Angola. Na wale woote wenye tabia ya kuuza madawa ya kulevya wasidhani tutakurupuka kuwasaidia hata kidogo ukifungwa fungwa tu, wakikulisha kinyesi kula tu, waki kurukisha kichura wewe ruka tu aise.

Anonymous said...

Mdau wa june 13,2013 at 8:50pm....Umeongea poa sana kabisa. Anabahati sana maana nchi nyingine unaruka na kifo kabisa kwa hiyo avumilie huko huko aliko. Mie napenda sana nchi zenye sharia kali na madawa ya kulevya. Afungwe kabisaaaaaaa tena hatutaki kusoma tena habari za huyu jamani, na ametoa waapi blackberry ya kutuma messege kwa raia? Naomba anyang'anywe hiyo simu ya mkononi kabisaaaa msoto msoto tu mpaka atie akili kuwa madawa ya kulevya NOMA.

Anonymous said...

Wote mmechemsha: ( kama MTanzania mwenzetu hatupaswi kumsaliti.. nini maana ya uzalendo? Ndugu wanaomba aje kutumikia kifungo nyumbani nyie kinawauma nini? Au tumesahau ni ukosefu wa ajira unaochangia biashara ya madawa? Kama raia wa Tanzania bila kujali yaliyomkuta uzalendo uwe kwanza!! Inasikitisha taifa limejaa wenye upeo mdogo kama hao hapo juu:( Sasa asipoomba kurejea nyumbani aende wapi? Mbona hatuwafukuzi wanaoiba mabilioni kila uchao? Unapokosa ukafungwa unarejea uraiani na jamii inakupa nafasi nyingine!! Aden Rage ni mbunge aliewahi kutumikia kifungo kwa kosa la wizi wa fedha... jamii imemsamehe na anajenga Taifa.. tuache umbumbumbu.

Anonymous said...

Wewe mdau wa June 14,2013 at 1:40 ..umeona Watu tumemsapoti mdau wa kwanza basi ukataka tu kupinga toa na wewe mawazo yako sio kuzungumzia wezi Kama rage, jamaa wa kwanza kaongea ukweli ndio maana tukakubaliana nae hata wewe ungeongea point tungeakubali ila unataka tu kupinga... Eti uzalendo kwa Watu wanaoumiza jamii ya Tanzania kwa madawa.... Sisi hatumjui Huyu mdau wa kwanza lakini Kama kaongea ukweli basi ukweli ni ukweli tu.

Anonymous said...

Wewe mdau uliyesema wote tumechemsha una matatizo katika akili yako au kama huna basi wewe nawe ni mteja kwa sababu huwezi kutetea ujinga na unaona vijana wa kitanzania wakiendelea kufa na wengine kuharibikiwa kutokana na hayo madawa, unatetea utanzania gani? je huyo anaye-supply madawa ni bora kuliko hao watanzania wanaolishwa madawa na kuangamia? Naomba ujiulize tu. KWANI UKOSEFU WA AJIRA NI JUSTIFICATION YA KUFANYA UHALIFU??? Amekosa ajira ili aharibu wengine nchi ilee vichaa siyo? Kuna picha hapo juu vijimambo kuna roho mbili za watanzania zinatakiwa zitolewe kwa ajili ya hiyo biashara ya madawa, haijulikani itatolewa lini...lakini kwa nchi hizo zenye kufuata sharia zake, WATANYONGWA TU, hakuna kuhonga huko, si ingekuwa nafuu wangeishi kwa kufanya kazi zilizo halali? Walishanyongwa watanzania huko Egypt miaka ya nyuma, Singapore wamenyongwa watanzania, China wamefungwa maisha na kwingineko watanzania wapo magerezani wakitumikia vifungo virefu....bado hamkomi tu?