SAKATA la Watanzania wawili waliokamtwa na dawa za kulevya nchini Misri imezidi kuwa na usiri mkubwa, baada ya ndugu zao kushindwa kupata ukweli juu ya uhai wao na tuhuma zinazo wakabiri.
Akizungumza na Mwanadishi wetu jijini Dar es Salaam ndugu wa karibu na watuhumiwa hao ambao ni mtu na binamu yake, alisema kwamba serikali ya Misri imeendelea kuficha ukweli wa suala la ngudu zake kukamatwa na dawa za kulevya.
"Bado tunahangaika kupata taarifa kamili juu ya maisha ya ndugu zangu, tumeweza kuwasiliana na ubalozi wa Misri nchini Tanzania wakasema kwamba hawana taarifa sahihi juu ya suala hilo, tukawasiliana na Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake nchini Misri, lakini taarifa tuliyopata ikatupa utata zaidi"alisema ndugu wa watuhumiwa hao kwa masharti ya kutotajwa jina lake mtandaoni.
Alisema kwamba "Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliweza kuwasiliana na Mamlaka zinazohusiana na kitengo cha dawa za kulevya na kukutana na watuhumiwa hao, ambapo walituwezesha kuzungumza nao kabla hawajapandshwa Mahakamani lakini baada ya hapo upatikani wa taarifa zao zimekuwa za siri sana" alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza:. Mpaka hivi sasa hatuelewi kinachoendelea,mawasilaino yamekuwa magumu ingawa hatujakata tamaa ya kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Misri"
Watuhumiwa hao wenye undugu wa mtoto wa Mjomba na Shangazi wakazi wa Magomeni na Ilala jijini Dar es Salaam ni Mbarak Abdallah (28) na Sharifa Mahmud (27), walikamatwa Mei 16 mwaka huu nchini humo wakitoka Jijini Dar es Salaa kupitia Nairobi nchini Kenya, wakiwa na dawa ya kulevya aina Heroine kilo saba. Baada ya kukamatwa Mei 18 mwaka huu Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliitwa kwenda kuwatambua na baada ya kubainika kwamba ni watanzania walirudishwa rumande baada ya kuzungumza na ndugu zao nchini Tanzania. Mei 26 walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande.
3 comments:
Muandishi tafadhali jufunze kuhakiki maandishi yako. Mara nyingi kwenye "L" unaweka "R" mfano Palestine umeandika "PaRestine", wakabili umeandika "wakabiRi".
may be mwandishi ni mtani wangu wa kule kashozi
bila shaka hata wewe anonymous unatakiwa kufanya uhakiki unapo andika kwani kwenye jifunze umeandika "jufunze" tuwe makini jamani sio kukurupuka na kurudia kula matapishi
Post a Comment