Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiukaribisha Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza uliowasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake.
Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni wao kutoka nchini Uingereza.
Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza umewasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake. Baada ya kupokelewa uwanja wa ndege wa Dodoma na Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, wabunge hao wakiwa na wenyeji wao walikutana na Makamu Mkuu wa UDOM Prof. Kikula na baadaye kufanya ziara fupi kwenye hospitali ya Chuo kitengo cha matibabu ya figo na sehemu ya utakasaji wa maji yanayotumika kwa upasuaji. Ziara ya UDOM iliitimishwa dhifa fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge ikiongowa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ngugai pamoja na Katibu wa TWPG na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki katika Hoteli ya Dodoma.
Chanzo: Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment