ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 14, 2013

Wassira: Ukuaji wa uchumi haufanani na uhalisia

Dodoma: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira amesema ukuaji wa uchumi hauendani na uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa kawaida.
Wassira aliyasema hayo Bungeni mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2012 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2013/14.
“Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja sasa, uchumi wa taifa umekuwa kwa wastani wa asilimia saba kwa mwaka lakini umaskini umepungua kwa kiwango kidogo cha asilimia mbili,” alisema Wassira ambaye taarifa yake iliwahi kutolewa na katika utafiti wa Benki ya Dunia, Februari mwaka huu kuhusu umaskini Tanzania.
Hata hivyo, alisema kwa mwaka 2013/14, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwezesha taasisi za wakulima wadogo kuinua kiwango cha ubora wa mazao, mifugo na uvuvi.
Kuwezesha makundi yenye umaskini uliokithiri pamoja na kupanua huduma za fedha vijijini ikijumuisha mikopo na bima, kuwezesha usindikizaji mazao na upatikanaji taarifa za masoko.
Akizungumzia maendeleo katika sekta ya uchumi, Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda, alisema katika kipindi cha nusu mwaka 2012/13, sekta zinazokua kwa kasi ni; madini, ujenzi, mawasiliano, biashara, utalii na huduma za fedha ambazo zina uwezo kuajiri Watanzania walio wengi.
Pia alisema shughuli za kiuchumi za kilimo, uwindaji na misitu kwa mwaka 2012, zilikuwa kwa asilimia 4.3 sawa na Viwanda na
Biashara zilizokua kwa asilimia 8.2 na zaidi ni udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato unaofanywa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA).
Mpango mwingine wa maendeleo ni kutandika bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kwamba maandalizi yake yameanza na jiwe la msingi liliwekwa tangu Novemba 2012.
Mwananchi

No comments: