ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 7, 2013

YANGA NAYO KUTOENDA DARFUR KUTETEA KOMBE LAKE


Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo cha karibu na uongozi wa klabu wa Yanga ni kwamba mabingwa hao watetezi wa kombe la Kagame hawatoenda kushiriki michuano hiyo mwaka huu iliyopangwa kuanza hivi karibuni huko Darfur Sudan.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya serikali kupitia wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kusema kwamba haioni busara kwa vilabu kwenda Darfur kwa sababu eneo hilo bado halina usalama wa kutosha - kauli iliyopelekea mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kusema kwamba timu yake haitokwenda Darfur kushiriki michuano hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa CECAFA na chama cha soka cha Sudan ni kwamba michuano hiyo itachezwa kwenye eneo lililo salama na lenye ulinzi mkubwa hivyo timu hazihitaji kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao pindi watakapoenda kushiriki michuano hiyo mapema mwezi ujao.
Hatua ya Yanga kujitoa inazidi kuongeza idadi ya vilabu ambavyo vimesema ikiwa michuano hiyo itafanyika Darfur basi havitashiriki Kagame Cup mwaka huu, vilabu vikubwa vya Sudan AL Hila na El Merreikh, Tusker ya Kenya na Simba SC vyenyewe vilishatangaza uamuzi wa kutokwenda Darfur kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments: