Barnaba
Fid-Q
Mira Nair1
Mrisho Mpoto
Tonya Lee Williams
Skylight Band
kwa picha zaidi bofya read more
TAMASHA LA 16 LA FILAMU LA KIMATAIFA/TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI - ZIFF
2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tamasha la 16 la Filamu la
Kimataifa/Tamasha la Nchi za Jahazi linategemewa kuanza mjini Zanzibar tarehe
29 Juni hadi 7 Julai, 2013. ZIFF
inawakaribisha sana kushiriki nasi katika siku hizi tisa za maonesho ya filamu,
utamaduni, kazi za mikono na burudani, tukiwa na imani kwamba fursa hii adhimu
itaweza kuwa nafasi nyingine tena katika kuenzi na kukuza Tamaduni zetu. Dhamira kuu ni kuhakikisha ZIFF inaleta
mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini, ZIFF pia imekua ikitoa ajira za
muda mfupi kwa washiriki wote, kuibua vipaji na kuzitangaza kazi mbalimbali za
sanaa na wasanii wa hapa nyumbani.
Kwa udhamini mkubwa kabisa wa
ZUKU kwa mwaka wa pili sasa tumeweza kuwafikia watengenezaji filamu wengi wa
Afrika Mashariki na kati ambako kote ZUKU wamekua wakitutangaza vyema. ZIFF
itaendelea kushirikiana na ZUKU kwa miaka mingine nane wakiwa ndio wadhamini
wakuu wa Tamasha.
FILAMU ZIFF 2013:
Wataayarishaji wa filamu zaidi ya
35 mahiri toka nchi mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia
ZIFF watahudhuria Tamasha hilo na pia watatumia fursa hiyo kuongelea filamu zao
na utengenezaji wa filamu kwa ujumla. Hii ni nafasi nzuri kwa watengenezaji filamu
wa hapa nyumbani kuhudhuria na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wenzao
toka nchi mbalimbali. Ikumbukwe zaidi ya Filamu 257 toka nchini mbali mbali
ziliwasilishwa mwaka huu, lakini ni Filamu 80 zilizofanikiwa kuchaguliwa
kuoneshwa na pia katika kushindania Tuzo za ZIFF. Tuzo zitolewazo katika ZIFF
ni Verona, Signis, Sembene, ZUKU na Tuzo za ZIFF. Tuzo za filamu za kitanzania
mwaka huu zimeshirikisha filamu 14 kutoka hapa Tanzania. Tuzo Kuu itolewayo
katika ZIFF ni Golden Dhow Award (Jahazi la Dhahabu).
Pia ZUKU itatoa tuzo kwa filamu
iliyotengenezwa na muongozaji wa kiafrika, imetengenzwa Afrika, imepigwa picha
Afrika na pia kuwatuza msanii bora wa kiume na kike.
VIKUNDI VYA BURUDANI ZITAKAZO SINDIKIZA TAMASHA LA 16 LA FILAMU- ZIFF
2013 ni pamoja na Mrisho Mpoto na Mjomba Band, Skylight Band, Linah, Fid Q,
Barnaba, Jhikoman, Baby J, Synerg, Swahili vibes, Safi theatre, Tongwa
Assembly(walimu wa chuo cha saa Bagamoyo), Mkubwa na wanawe(Said Fela), kundi
la Shiwe kutoka Comoro na makundi mengine mengi kutajwa hapo baadae.
JUKWAA LA WATOTO - CHILDREN PANORAMA, mwaka huu ni tofauti na miaka
iliyopita, jukwaa hili litahusisha watoto toka nchi tatu za Afrika Mashariki,
Uganda, Tanzania na Kenya. Jukwaa hili litatoa nafasi kwa filamu za watoto
kuoneshwa katika kipindi cha Tamasha na litawafikia wanafunzi zaidi ya 1500
kutoka shule za msingi na sekondari za
Zanzibar pia kutakuwa na Warsha Mafunzo (Workshop) juu ya utengenezaji wa
Katuni (Animation) – Warsha hii imedhaminiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
- Zanzibar.
JUKWAA LA VIJIJINI - VILLAGE PANORAMA, jukwaa hili litahusisha
vijiji 10 vya Unguja na 3 vya Pemba, kutakuwa na Filamu zitakazooneshwa pamoja
na warsha mbalimbali za wakinamama na Watoto na Afya ya Uzazi salama.
JUKWAA LA KINAMAMA - WOMEN PANORAMA, jukwaa hili mara nyingi
huambatana na jukwaa la Vijijini, Kutakuwa na Warsha juu ya wanawake na uzazi
salama, Kutakuwa na Warsha juu ya unyanyasaji wa kijinsia sehemu ya kazi na
Kutakuwa na Warsha juu ya wanawake, filamu na afya na litadhaminiwa na
PSI/UNFPA.
MAONESHO (EXHIBITIONS) “SOKO FILAMU", Mabanda ya maonesho
mbalimbali ya kazi za sanaa za mikono na ubunifu (Made in Tanzania), wakati
Tamasha SOko-Filamu hutoa fursa kwa watu kununua na kuuza kazi za mikono pamoja
na kutengeneza mitandao ya kibiashara.
Kutakuwa na banda Maalum la ZUKU ambalo litatumika kama sehemu maalum ya
kuuza ving’amuzi lakini pia ni sehemu ya kununua kazi za wasanii (filamu).
MASHINDANO YA MBIO ZA JAHAZI (DHOW RACE) KUFANYIKA TAREHE 30 JUNE, Majahazi
10 yaitashiriki katika mashindano ya Mbio za Majahazi Baharini, ambapo mshindi
atazawadiwa wa kwanza atapata 200,000, Mshindi wa pili 150,000 na Mshindi wa
tatu 100,000 za Kitanzania na Mashindano haya ni kwa Udhamini Mkubwa wa
Zanzibar Connection.
Mwaka huu tuna Warsha Mafunzo (Workshops) zifuatazo: -
·
Watoto – Utengenezaji Katuni (Animation)
·
Juigiza katika Kamera (Acting for Camera)
·
Uandishi Habari za Sanaa (Arts Journalism)
·
Uandishi wa Miongozo ya Filamu (Script Writing)
·
Utengenezaji Filamu (Film production)
·
Uandishi Chambuzi (Critical Journalism)
·
Malaria & HIV- Pemba
KONGAMANO – Juni 28 hadi Juni 30, mwaka huu kutakuwa na Kongamano
maalum la “Bongo Movie Symposium” litakaloendeshwa na Murdoch University
kuanzia tarehe 28-30 June na litajadili kitabu kinachohusu Bongo Movie ambacho
kimehaririwa na Prof Martin Mhando.
FASHION SHOW – Juni 29, Kwenye uwanja wa Mitindo Tamasha la 16 la
filamu Tanzania ZIFF kutakuwa na onesho maalum la mavazi zitakalo ongozwa na
Mustafa Hassanali, Farouque Abdella na Javed Jaffary mnamo tarehe 29 June.
FESTIVAL OF FESTIVALS – Juni 30 hadi Julai 6, hii huwa ni fursa ya kujitangaza kibiashara
katika ZIFF na mwaka huu kutakuwa na Iran, Australia, South Africa, ZUKU na
TANAPA kila siku kuanzia saa 8 mchana – 11 jioni katika Ukumbi wa Maru Maru
Hotel. Ila Mwaka huu ZUKU watachukua Fursa hii kukutana na watengenezaji filamu
wa kitanzania na kujadili soko la filamu Tanzania na pia kununua kazi za
watengenezaji filamu wa kitanzania.
SIKU MAALUM YA FILAMU ZA KIBONGO - SWAHILI DAY – Julai 5, Filamu 14
kutoka Bongo Movie zitaoneshwa kuanzia asubuhi hadi jioni kila siku katika
kumbi maalum ili kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kuona kazi za nyumbani. Siku
ya tarehe 5 ni siku maalum imetengwa kama muendelezo wa ZIFF kuonesha kujali
kilicho cha kwetu, filamu za Kiswahili zitaoneshwa katika jukwaa kuu na pia
kuwakaribisha wasanii mbalimbali kuhudhuria Tamasha na kupata nafasi ya
kukutana na watengenezaji filamu wengine nia na madhumini ni kuzipa kipaumbele
na kuenzi kazi za filamu za wasanii wa Kitanzania.
USIKU WA TUZO (AWARD NIGHT) - Julai 6, Tuzo zitatolewa kupitia
Filamu 80 zinazowania Tuzo mbalimbali katika Tamasha la 16 la filamu ZIFF 2013
na MWISHO WA TAMASHA ni Julai 7
MGENI RASMI (CHIEF GUEST), mwaka huu mgeni wetu maalum atakua Tonya Lee Williams, muigizaji
Muingereza ambaye amecheza tamthiliya kubwa Marekani ya The Young and the
Restless na the Bold and the Beautiful, pia
Tonya atafanya warsha ya uigizaji katika ZIFF.
FILAMU YA UFUNGUZI, mwaka huu filamu ya “The Reluctant Fundamentalist” kutoka kwa mtengeneza filamu maarufu
na mwanzilishi wa Maisha Film Lab, MIRA NAIR ndiyo itakua filamu ya ufunguzi na
filamu hii imetengenezwa nchini Marekani, India na Sweden.
WADHAMINI WETU 2013 ni: -
·
Zuku –Mdhamini Mkuu
·
Azam Marine
·
Ethiopian Airways
·
Prime Time Promotions
·
GIZ
·
Goethe Institute
·
German Cooperation
·
TMF
·
Murdoch University
·
Zanzibar Beach Hotel
·
Zanzibar Connection
·
Zanlink
·
Grand Palace Hotel
·
Maru Maru Hotel
·
Wavuvi Restaurant
·
WIOMSA
·
PSI
·
UNFPA
·
Visual Media Institute - Iran
TUNAPENDA PIA KUTAMBUA MCHANGO WA SERIKALI YA ZANZIBAR NA YA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
No comments:
Post a Comment