MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na wanaume ambao hawana hela lakini wamekuwa wakijifanya wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza.
Akiongea na mwandishi wetu , Kabula alisema anajua kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni wanaume wasio na kitu.
“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo, wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao kifedha zaidi ya kuonesha wana wivu na wakipishana kidogo tu kipigo kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula.
2 comments:
Huyu binti anasema hawapendi wanaume wenye wivu wakati hawana hela. Tafsiri yake ni kuwa mwanaume wake akiishiwa hela ni lazima atafute wanaume wenye hela na asiulizwe swali. Kwa mantiki hiyo basi, binti huyu hapendi mtu, bali anapenda hela. Jinsi ninavyo fahamu mimi na pengine wadau wengi ni kuwa kitendo cha kufanya mapenzi ili kupata hela ni umalaya. Na mtu anayefanya umalaya, anajulikana kama Malaya. Kwahiyo huyu binti ni Malaya. Kama nimekosea naomba kusahihishwa.
Hujakosea kabisa
Post a Comment