ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

JOYCE KIRIA ASIMULIA JINSI ALIVYOFANYA KAZI KAMA HOUSE GIRL KWA MIAKA MIWILI

Je! Wajua kuwa mtangazaji maarufu wa TV nchini Joyce Kiria aliwahi kuwa mfanyakazi wa ndani jijini Dar es Salaam? 
Mtangazaji huyo mrembo wa kipindi cha Wanawake Live amesimulia kwa ufupi sababu zilizompelekea kuja jijini Dar es Salaam na kufanya kazi za nyumbani kwenye kipindi cha wiki hii cha Fema Radio Show kinachotayarishwa na shirika la FeminaHIP na watangazaji wakiwa Michael Baruti na Rebecca Gyumi.

“Mtu aliyenishawishi ni baba yangu mzazi, Mungu amweke mahali pema peponi, na nililia sana alivyoniambia niende Dar es Salaam nikafanye kazi za nyumbani,”alisema Joyce Kiria.
“Mimi binafsi nilikuwa napenda sana kuendelea na masomo na si kwamba najisifia lakini tangu nimeanza darasa la kwanza mpaka darasa la saba nimekuwa ni mtoto wa kwanza wa pili. Kwahivyo nikawa na matumaini makubwa kwamba ntaendelea kielimu sana tu. So nilipokuja kufika darasa la saba na nikaona maisha ya wazazi wangu yamezidi kubadilika, kwasababu baba yangu alikuwa anaishi Tabora na alikuwa ni mfanyabiashara tu mzuri. Lakini maisha yalianza kumbadilikia nikiwa sijamaliza shule. Mpaka namaliza darasa la sababu alikuwa almost amefilisika na amerudi kijijini kwahiyo kukawa hakuna na njia yoyote ya kuendelea na shule.”

Joyce amewapa ushauri vijana wanaomaliza shule kuzingatia masomo na kutopenda kukimbilia jijini Dar es Salaam kwakuwa maisha si rahisi.

“Watu wengi wakimaliza darasa la sababu wanaanza kufikiria kukimbilia Dar es Salaam na miji mikubwa au hata kabla hajamaliza shule kuna wengine wanatoroka hata kabla ya hapo.

2 comments:

Anonymous said...

Maisha ndivyo yalivyo, kumbuka baada ya dhiki FARAJA.
hongera hapo ulipo.

Anonymous said...

Mrembo, du!