ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 4, 2013

MHE. ALI HASSAN MWINYI AWASILI WASHINGTON, DC TAYARI KWA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI NA SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO

 Mhe. Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi akishuka kwenye gari akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa Dulles Sterling, Virginia Mhe. Mwinyi amekuja kwa ajili ya Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Blog ya Vijimambo litakalofanyika Jumamosi July 6, 2013.
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa habari Mindi Kasiga wakati alipokua akiingia Hotelini.
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa Ubalozi Bwn. Mwafongo huku Kaimu Balozi Mama Lily munanka akiwatambulisha.
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV na mwanakamati wa kamati ya maandalizi ya miaka 3 y.a Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Katibu wa kamati ya maandalizi, Asha Nyang'anyi.
 Juu na chini ni Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na watoto watakaompa maua.
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na katibu msaidizi Bwn. Julius Katanga, na Masanja Mkandamizaji akiwatayari kusalimiana na Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana akisalimiana na Shilole.
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akipokea maua toka kwa Munirah
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na Brian, na Munirah, watoto waliowapa maua.

Picha zingine baadae

3 comments:

Anonymous said...

Jamani huyu ni sitty au bi khadija?
mtazamo wangu huyu ni mama khadija mwandishi hebu nifanunulie vyema kimtazamo...isiwe macho yangu na huyu mama siki ni nyingi..

Anonymous said...

mwandishi huyu ni mama sitti mwinyi au mama Khadija? hebu nifanulie vizuri hii sura labda macho yangu? ni siku nyingi mwanadamu hubadilika au vipi waungwana..


.

Anonymous said...

Huyu ni mama Sitti Mwinyi.