ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 4, 2013

UWOYA AJICHORA MAKANYAGIO YA MWANAE MGOGONI

Staa wa muvi za Bongo, Irene Pancras Uwoya ameonesha upendo wake kwa mwanaye Krrish Ndikumana kwa kujichora ‘tatuu’ mgongoni yenye nyayo (makanyagio) ya mtoto huyo na kuzisindikiza na jina lake kwa juu.

Baada ya mchoro huo kukamilika, Uwoya aliitumbukiza kwenye mtandao wake wa kijamiii wa Facebook na kutazamwa na watu kibao ambao waliipenda.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi wetu kuhusiana na tatuu hiyo walisema Uwoya amefuata nyayo za wanawake wengi wa Kiafrika ambao wakishazaa huwapenda sana watoto kuliko baba zao.

“Picha ni nzuri, mama ameonesha upendo wake kwa mtoto lakini hii ni tabia ya wanawake wengi wa Kiafrika, wakishazaa mapenzi yote wanayahamishia kwa watoto badala ya waume zao.

“We fuatilia utagundua ndoa nyingi huanza kuyumba baada ya mke kujifungua, maana mapenzi yote yanahamia kwa mtoto, mume kama hana subira anaanza kutafuta mwanamke mwingine wa kumpenda upya.
“Inawezekana Uwoya mwilini mwake hana tatuu hata moja ya mumewe, lakini Krrish kamchora nyayo ili kuwaoneshea wadau wake,” alisema Oscar Samuel, mkazi wa Mwenge, Dar.

No comments: