Thursday, July 18, 2013

MWANAHABARI MAJEBELE AZIKWA

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamelibeba sanduku lililohiofadhi mwili wa Marehemu David Majebele wakienda kuzika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Majebele ni miongoni mwa waandishi wa Habari wakongwe wa Tanzania waliokuwa wakifanya vyema katika tasnia yao kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa makaburini wakati wa mazishi ya Mzee David Michael Majebele.
Baadhi ya watoto wa Marehemu wakiwa makaburini.
Wanafamilia ya Majebele wakiwa na simanzi wakati wa kukamilisha safari ya mwisho ya ndugu yao.
MWILI wa mwandishi mkongwe David Michael Majebelle. aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita umezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.

Kabla ya mazishi hayo ulipelekwa nyumbani kwake eneo la Sinza jirani na Lion Hotel ambapo heshima za mwisho zilitolewa majira ya saa sita mchana kisha kulepekekwa katika kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi lililopo Sinza na baadaye makaburi ya Kinondoni.

Marehemu Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.

No comments: