ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 17, 2013

NI SABABU GANI WANAOTOKA AFRIKA HUSUSANI TANZANIA HUCHELEWA KWENYE MIALIKO?


Na Deusdedit Mntali
Kwa wanaotoka Afrika hususani Tanzania nina masikitiko makubwa sana kwa Waafrika na tabia hii imezidi sana kwa Watanzania kwa kuchelewa kwenye mialiko bila kujali umuhimu wa mualiko. Tabia hii inabiti ipatiwe ufumbuzi tujaribu kufanya majadiliano ya jinsi gani ya kukomesha tabia hii.

Ni juzi kati tu kwenye sherehe ya Vijimambo Mhe. Ali Hassan Mwinyi ilibidi achelewe kuingia ukumbini kutokana na waalikwa wengine kuchelewa kufika kwenye muda uliopangwa japo tupo ughaibuni lakini inaonesha tulisahau kurekebisha saa zetu wakati tunavuba bahari ya Atlantic.

Nikitu gani hasa kinachotufanya kuchelewa tunapoalikwa bila kujali aliyetualika kalipia ukumbi kwa muda maalum, Watanzania wenzangu na wenzangu kutoka Afrika tunamatatizo gani na muda?. Kuna waalikwa wengine hujaribu kupiga simu kwa waliotangulia kujaribu kuuliza kama kuna watu tayari ukumbini bila kutumia akili kwamba wao pia ni moja ya walioalikwa wanaotakiwa kuwahi ili ukumbi ujae na mualika aanze shughuli yake kwa muda muafaka na muda uliopangwa.

Nawapongeza wale wote wanaoanza shughuli yao bila kujali kuna watu au hakuna tukiwa wote na msimamo huu nadhani kwa kiasi kikubwa tutawafunza wachelewaji wote waweze kuwahi wanapoalikwa na nafikiri hata chakula kikishaliwa kiondolewe mezani ili iwefunzo kwa wachelewaji wote.

 Pia na walaani wale waalika wote wanaochelewa kwenye shughuli zao sijui tuwafanye nini hawa, shughuli yako mwenyewe na bado unachelewa waalikwa wanafika wanajikuta wenyewe hii ni kali sijui tufanyeje kuikomesha hii ningekua mimi ndio ningeondoka bila hata kujali ukaribu wa mualika kusudi atakapofika ajikute peke yake siku nyingine atawahi.

 Ni hayo tu kwa leo.
 Mdau DMV.

7 comments:

Anonymous said...

YAANI KWENYE MAHARUSI KUCHELEWA NDIO KILA MARA! BWANA NA BIBI HARUSI WANASEMA HARUSI NI SAA MBILI USIKU LAKINI WAO WANAFIKA SAA SITA USIKU!!! YAANI WATANZANIA HATUJIFUNZI KITU IKIJA KWENYE MUDA.




Anonymous said...

Mie naona ni Madharau tu. Hakika kama unajiheshimu wewe binafsi lazima utaheshimu wengine. Maana sioni cha zaidi hapa ya MADHARAU Yaliyo kithiri. Maana visingizio vya (1) Nakaa mbali (2)Traffic mbaya sana (3)matengenezo ya barabara (4) Nimepitia kumchukua Fulani na Fulani hiviiiiii visingizio vyooooooote vimepitwa na wakati sana tu, hakuna jipya. MADHARAU NA MAKIDAI ndo yanasababisha mtu kwenda kwenye shughuli ya mtu muda anao jisikia.

Anonymous said...

Mmoja liliosemwa ni kweli, MADHARU. Kudharau Watanzania wenzako na utamaduni wa Kiafrika ni tokeo. Lakini ini la swali ni KWA NINI KUNA MADHARAU KAMA HAYA ? Hili swali inabidi tulitafiti. Fikiri ! Watu hao hao wanaochelewa kuja kwenye mialiko, mbona wanapoenda kazini hutochelewa ? Hasa wale wanofanya kazi mwenye masharika yasio ya KiTanzania. Fikiri tena, hapa wale wanaofanya kazi kwenye Domino Pizza au McDonald, hawachelewi kufika kazini.Ni Time Card inawashurutiza ?

Kazini hutochelewa, kwenye shuguli za WaTanzania kuchelewa ni tabia. Kwa nini tuna madharau ?

Kama mwenzangu hapa alivyoeleza, kukomesha tabia hii ni kuanza shuguli wakati uliyopangwa na kuimaliza wakati uiyopangwa.

"Chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako". Kwa kisasa tuseme, "Chelewa chelewa wakati utakutwanga".

Asanteni.

Mwalimu A.

Anonymous said...

mbona shughuli za wazungu tunawahi hata kama tunakaa mbali? mie nilishaacha kualika wabongo kwenye shughuli zangu. maana unaandaa kila kitu unakaa mkao wa kupokea wageni unakuta mijitu inachelewa 3 hours, dinner gani ya kula saa sita usiku? I JUST HATE THE WAITING GAME, inaharibu hata ladha ya shughuli mscheeew

Anonymous said...

juzi juzi kulikuwa na party pale MLK tukaambiwa inaanza 7pm. hadi midnite ndo mhusika anaingia. by then nilikuwa nishaanza kupiga miayo nikaishia zangu home. halafu kesho yake watu eti ooh party ilikuwa nzuri

Anonymous said...

Binafsi sina tabia ya kuchelewa sana kwenye sherehe,lakini kama wadau walivyosema hapo juu,unafika ukumbini unakaa masaa 2 hata 3 sherehe haijaanza. Kumbuka hapo labda umeacha watoto kwa babysitter unalipia kwa masaa, unapoteza muda kung'aa macho ukumbini... hali kama hiyo nadhani inapelekea watu kuamua kuchelewa makusudi ili angalau wakifika sherehe ishaanza. Kwa hiyo nadhani mwandaaji wa sherehe akizingatia muda, naamini na waalikwa nao watazingatia muda.

Anonymous said...

watanzania inabidi tubadilike especially wa DMV. mtu unawaalika watu kwenye party halafu unawagandisha for four hours! that is so DISRESPECTFUL! nakumbuka ile shughuli ya DICOTA mwaka ulee kila kitu kilianza on time sababu wahudhuriaji wengi walitokea nje ya DMV. nimegundua watanzania wa states zingine wana-keep time. hapa DMV kumejaa tu majungu, ukosoaji, kutokupendana, kutokujaliana. every body is talking bad about every body hadi inatia hasira.