ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

RAIS KIKWETE KUWA REFA MECHI YA WABUNGE NA MGENI RASMI TAMASHA LA MATUMAINI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Na Mwandishi Wetu
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.
Eric Shigongo.
Akizungumzia zaidi juu ya ugeni huo mkubwa, Mrisho alisema: “Rais Kikwete amekubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi, atatumia nafasi hiyo kutoa neno la matumaini kwa wote watakaojitokeza uwanjani hapo.
“Rais pia ndiye atakayefungua mechi ya Wabunge wa Simba dhidi ya Yanga ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa. Kama ujuavyo rais wetu ni mtu wa watu na ni mpenda michezo, hilo linajulikana siku zote.”

Aidha, Mrisho aliongeza kwa kusema kuwa shabaha ya tamasha hilo ni kuamsha upya imani ya Watanzania kwa nchi yao. Kuwafanya wawe wazalendo na kila mmoja kujiona analo jukumu la kufanya, kuhakikisha Tanzania yetu inapiga hatua.“Mbali na Rais Kikwete, wengine watakaotoa neno la matumaini siku hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.

Zitto Kabwe.

“Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya East Africa Speakers Bureau Limited (EASB), Paul Mashauri, mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali, James Mwang’amba na mwanamitindo, Jokate Mwegelo.
“Wote hao, kila mmoja atakuwa na fursa ya kufikisha Neno la Matumaini ili kila atakayehudhuria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, aondoke akiwa mpya, akiwa na matumaini mapya kwa taifa lake na maisha yake kwa jumla,” alisema Mrisho.
Nape Nnauye.

Kwa upande wake Shigongo amesema kuwa udini, ukabila na kila aina ya ubaguzi, vitachimbiwa shimo na kuzikwa.
“Taifa linapita kwenye kipindi kigumu ambacho ni changamoto nzito. Unazungumzwa ufisadi, migomo imekuwa mingi, udini na ukabila vinapenyezwa kwa kasi, pamoja na aina zote za ubaguzi, hivi vyote tunapaswa kuvizika.
“Tuna makusudio ya kuwafanya Watanzania wajione wamoja licha ya tofauti za kiitikadi zilizopo. Mahitaji yetu ni kupaza sauti kuwa kila mtu yupo huru kusimamia anachokiamini lakini linapokuja suala la umoja wa kitaifa, tofauti zote zinapaswa kuwekwa kando,” alisema Shigongo.
Paul Mashauri.

Akizungumzia juu ya tamasha hilo, Shigongo alisema: “Hivi karibuni matokeo ya kidato cha nne yalitoka hapa nchini na kuonyesha watoto wengi walikuwa wamefeli. Kilichoniuma zaidi ni niliposikia baadhi ya watoto waliamua kukatisha maisha yao kwa sababu matokeo yao yalikuwa mabaya.”

1 comment:

Anonymous said...

Hiyo kwa kweli ndiyo kitu tunataka kusikia kutoka kwenu Shigongo and company. Inatia moyo kusikia kuwa sasa kuna watu mmeliona hilo. Na mko tayari kuondoa hayo yote kulinda sifa ya utaifa wetu. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wote. Asanteni jamani.