ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

VIJANA DMV YAIFUNGA KWA TAAABU VETERAN DMV GOLI 7-4, SAIDI MWAMENDE NYOTA WA MCHEZO

DMV Veteran wakijadili jambo

 Timu ya Vijana DMV Jana alhamisi July 4, 2013 walidhihirisha ubabe wao kwa kuwafunga timu ya DMV Veteran kwa goli 7-4 katika mechi iliyopigwa Heurich Turf Field, Hyattsville, Maryland na kuhudhuriwa na mashabiki wa DMV na kutoka majimbo mengine waliofika kwa ajili ya Tamasha la utamaduni wa Kiswahili na Sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo.
 Timu ya DMV Veteran

Mpambano ulianza taratibu huku Vijana DMV wakipiga pasi fupi fupi mithili ya Barcelona huku wakiongozwa na Libe German Diffence na kuwafanya DMV Veteran kuchanganyikiwa. Safu ya ushambuliaji ya Vijana DMV ilikua butu hasa kipindi cha kwanza baada ya kukosa magoli ya wazi kwa kupiga mpira nje au kumlenga kipa.
 Timu ya Vijana DMV

Kunako ddk 39 kipindi cha kwanza Mussa Linga aliiandikia DMV Veteran Bao la kwanza, bao lililotia hamasa kwa Vijana DMV na kuanza kushambulia kama nyuki na kupelekea kuswazisha katika ddk ya 43 kwa mchezaji Chris Muhoka akifunga goli rahisi kwa mabeki wa DMV Veteran wakidhani ameotea.
 Timu Kepteni wa timu zaote mbili wakipata mawili matatu kutoka kwa refa

Mpaka mapumziko timu zote zilikua droo ya 1-1 kipindi cha pili DMV Veteran waliwapumzisha Idd Sandaly na kumuingiza Danny Star ambaye alionekana Mwiba kwa Vijana kwani aliipashida kwa pasi ndefu alizotoa kwa wachezaji wenzake lakini umaliziaji ulikua mbovu.
 Mchezaji Chris akiambaa na mpira.

Kunako ddk ya 55 Vijana walipata bao 2 bao ambalo liliamsha nguvu ya Vijana na kuanza kulishambulia timu ya DMV Veteran kama nyuki na juhudi hizo zilizaa matunda kwa timu ya Vijana kujipatia mabao ya haraka haraka ddk 66, 68, 70, na kunako ddk 76 mchzaji Chriss alikwatuliwa ndani ya 18 na kusababisha penati lilypigwa kiufundi na Roger na kuiandikia Vijana bao la 5.
 Ismail akiamba na mpira.

Kunako ddk ya 80 Musa Linga aliandikia DMV Veteran bao la 2 kabla ya Beach Boy kufunga bao la 3 kunako ddk ya 83. na kunako ddk ya 86 Vijana walipta bao la 6 mfungaji akiwa Hussein aliyechanbua ngome ya Veteran na kuachia shuti kali lililomshinda golikipa Saidi Mwamende amabe mechi ya jana alikua nyota wa mchezo kwa kukata magoli mengi ya wazi ya timu  ya Vijana bila yeye kuwepo golini ubaoa wa magoli huenda ungesomeka vingine.
 Mchezaji David Ndunguru akiipatia Vijana bao

Kunako ddk 88 DMV Veteran walifunga kitabu chao cha magoli kwa kupachika bao la 4. dakika zilivyokua zikiyoyoma Vijana nao ndio walikua kama kwamba ndio asubuhi walizidi kuliandama lango la wazee kama nyuki na kasababisha goli lingine kunako ddk 89 likiwa limefungwa na David Ndunguru ambaye yeye na Chris Muhoka walikua mwiba kwa timu ya DMV Veteran.
 Nyota ya mchezo Said Mwamende akiokota mpira wavuni

Mpaka ddk 90 Vijana DMV waliibuka washindi kwa kuibamiza DMV Veteran kwa goli 7-4.
 Makeo akimzunguka Jabir Jongo
 Juu na chini mashabiki na wachezaji wa DMV Veteran

No comments: