ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 3, 2013

MAKALA: USAJILI WA GARETH BALE UNAASHIRIA SIKU ZA CRISTIANO RONALDO KUBAKI SANTIAGO BERNABEU ZIPO SHAKANI


Wakati Real Madrid wakiwa kwenye harakati za kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili winga wa Tottenham Gareth Bale, uhamisho ambao unatoa ishara kwamba mwisho wa mchezaji waliyemlipia fedha nyingi zilizovunja rekodi ya dunia Cristiano Ronaldo unakaribia? Imekuwa ikiaminika kwamba Madrid wangeenda kumnunua Bale msimu huu ikiwa tu Ronaldo atataka kuondoka. Kwa sasa, mreno huyo anabaki kuwa mchezaji wa Real Madrid kwa asilimia mia, lakini kwa namna Madrid inavyoonesha kumhitaji Bale inaonekana siku za Ronaldo Bernabeu ni za kuhesabika.

Wakati tetesi za Ronaldo kurudi Manchester United ambazo zilitikisa sana mwanzoni mwa dirisha la usajili, sasa zinaonekana zimepoa, bado hatma yake ndani ya Madrid ipo shakani. Sababu kuu la hilo ni kwamba winga huyo mwenye miaka 28 anaingia kwenye miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake, hatua ambayo thamani ya mchezaji huanza kushuka, na ameonyesha hana nia ya kusaini mkataba mpya. Mara ya mwisho Ronaldo kuzungumzia mkataba wake na Madrid alisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba 'taarifa zote za kusaini mkataba mpya ni za uongo'.

Huko nyuma, Ronaldo alizipa tetesi za kutaka kuondoka baada ya kusema kwamba hakuwa na furaha kwa sababu za kikazi ndani ya Madrid, kitu kilichotafsiriwa kwamba alikuwa akihitaji mashahara mkubwa na sapoti kubwa kutoka viongozi wa juu wa klabu. Mtu mmoja ambaye haamini kama suala hilo lilishaisha ni raisi wa zamani wa Madrid Ramon Calderon.

"Nafahamu kwamba hana furaha kabisa kwasababu ya tabia za Raisi," aliiambiaTalksport Jumatano iliyopita. “Anataka mshahara wa €20 million kwa msimu jambo ambalo litakuwa gumu kwa Real kukubali.”

Na Calderon pia anaamini kwamba uhamisho wa kumleta Bale umechangiwa sana na sintofahamu ya hatma ya Ronaldo. “Nadhani raisi amejiandaa kwa kila kitu ikiwa atashindwa kumshawishi Ronaldo asaini dili jipya. Hivyo ndivyo ninavyoona. Anaogopa utafikia wakati Cristiano atasema 'sitaki kuendelea kuwa hapa'. Hiyo itakuwa habari mbaya kwa Madrid. Ningependa aendelee kuwa pale na kustaafu soka akiwa Bernabeu lakini kwa sasa hali ilivyo ni vigumu. Ngoja tuone wiki kadhaa zijazo mambo yatakavyokuwa.”


Maoni ya Calderon ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa kumleta Ronaldo Madrid - na amekuwa akimtuhumu Perez kwamba kutokana hakuhusika katika kumleta mchezaji huyo ndio sababu ya kutompa sapoti mchezaji anayohitaji tofauti na ilivyo kwa wachezaji ambao alihusika na kuwanunua moja kwa moja, kitu ambacho kimewahi kumtokea hata Gonzalo Higuain.

wanaweza kumuuza kwa kiasi kidogo au wakakosa kabisa ikiwa atabaki mpaka mkataba wake utakapoisha.

No comments: