Wapendwa wana CCM, itakumbukwa mnamo tarehe June 3, 2013 Tume ilitangaza Rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hatua hii ya mwanzo ya kukamilika kwa katiba mpya ni sehemu ya kwanza ya kukamilika kwa katiba. Pia, ikumbukwe hatua ya pili ni kuwasilishwa rasimu ya pili kwenye Bunge la Katiba. Mwisho, kutakuwa na Rasimu ya tatu itakayofikishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Wana CCM, hatua hii ya pili ya tume ya katiba ni kwamba inajadiliwa katika mfumo wa mabaraza ya asasi na vyama vya siasa. Kwa kuzingatia kwamba chama cha mapinduzi ni taasisi muhimu na yenye maslahi makubwa katika upatikanaji wa katiba mpya.
Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ilikutana mjini Dodoma tarehe October 6,2013 ilitoa maamuzi ya kwamba uandaliwe ufafanuzi utakaorahisisha utoaji wa maoni utakaotumiwa na wana ccm katika kutoa maoni.
Madhumuin ya mpango huu ni kuwawezesha wana CCM kushiriki na kutoa maoni yao kikamilifu kutoka ngazi ya matawi hadi Taifa.
UTARATIBU WA KUTOA MAONI
Tawi la CCM- Washington DC, Maryland & Virginia litapokea maoni ya Rasimu ya katiba kwa njia ya mawasiliano ifuatayo:
dmvccm@gmail.com
Tafadhali, mwana CCM tawi la DMV toa maoni yako kwa uhuru na ni haki yako kufanya hivyo juu ya rasimu ya katiba.
Utaratibu wa kutoa maoni, juu ya Rasimu ya kwanza ndani ya chama cha mapinduzi, wanachama wanaelekezwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
1. Kuitaja sura ya Rasimu ya Katiba inayohusika
2. kutaja ibara ya Rasimu ya katiba
3. Kutoa maelezo juu ya Ibara hiyo kama kuna upungufu au uhuru wa kutoa maoni mengine yoyote
4. Mapendekezo ya Marekebisho
5. Sababu za mapendekezo ya marekebisho hayo
SURA ZA RASIMU YA KATIBA KWA MUHTASARI
SURA, SEHEMU NA KILA SEHEMU INA IBARA
SURA YA KWANZA
Sehemu:Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mipaka, Alama, Lugha, Utamaduni na Tunu za Taifa
SURA YA PILI
Mamlaka ya wananchi, Utii na Hifadhi ya Katiba
SURA YA TATU
Maadili na miiko ya Uongozi wa umma
SURA YA NNE
Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia na Mamlaka za nchi.
No comments:
Post a Comment